Text copied!
CopyCompare
Biblia ya Kiswahili - Wagalatia

Wagalatia 3

Help us?
Click on verse(s) to share them!
1Wagalatia wajinga, ni jicho gani ovu lililowaharibu? Je Yesu Kristo hakuoneshwa kama msulubiwa mbele ya macho yenu?
2Mimi nataka tu kufahamu hili kutoka kwenu. Je mlimpokea Roho kwa matendo ya sheria au kwa kuamini kile mlichosikia?
3Je, ninyi ni wajinga kiasi hiki? Je mlianza katika Roho ili mmalize katika mwili?
4Je mliteseka kwa mambo mengi bure, kama kweli yalikuwa ya bure?
5Je yeye atoaye Roho kwenu na kutenda matendo ya nguvu kati yenu hufanya kwa matendo ya sheria au kwa kusikia pamoja na imani?
6Abraham “Alimwamini Mungu akahesabiwa kuwa mwenye haki”.
7Kwa namna ile ile eleweni kwamba, wale ambao wanaamini ni watoto wa Abrahamu.
8Andiko lilitabiri kwamba Mungu angewahesabia haki watu wa mataifa kwa njia ya imani. Injili ilihubiriwa kwanza kwa Abrahamu: “katika wewe mataifa yote yatabarikiwa”.
9Ili baadaye wale ambao wana imani wabarikiwe pamoja na Abrahamu, ambaye alikuwa na imani.
10Wale ambao wanategemea matendo ya sheria wako chini ya laana. Kwa kuwa imeandikwa, “Amelaaniwa kila mtu ambaye hashikamani na mambo yote yaliyoandikwa katika kitabu cha sheria, kuyatenda yote.”
11Sasa ni wazi kwamba Mungu hamhesabii haki hata mmoja kwa sheria, kwa kuwa “Mwenye haki ataishi kwa imani”.
12Sheria haitokani na imani, lakini badala yake “Ambaye hufanya mambo haya katika sheria, ataishi kwa sheria.”
13Kristo alitukomboa sisi kutoka katika laana ya sheria wakati alipofanyika laana kwa ajili yetu. Kwa kuwa imeandikwa, “Amelaaniwa kila mtu aangikwaye juu ya mti.”
14Lengo lilikuwa kwamba, baraka ambazo zilikuwa kwa Ibrahimu zingekuja kwa watu wa mataifa katika Kristo Yesu, ili kwamba tuweze kupokea ahadi ya Roho kupitia imani.
15Ndugu, ninazungumza kwa namna ya kibinadamu. Hata wakati ambapo agano la kibinadamu limekwisha kuwekwa imara, hakuna awezaye kupuuza au kuongezea.
16Sasa ahadi zilisemwa kwa Ibrahim na kwa kizazi chake. Haisemi, “kwa vizazi,” kumaanisha wengi, bali badala yake kwa mmoja pekee, “kwa kizazi chako,” ambaye ni Kristo.
17Sasa nasema hivi, sheria ambayo ilikuja miaka 430 baadaye, haiondoi agano la nyuma lililowekwa na Mungu.
18Kwa kuwa kama urithi ungelikuja kwa njia ya sheria, usingekuwa tena umekuja kwa njia ya ahadi. Lakini Mungu aliutoa bure kwa Ibrahimu kwa njia ya ahadi.

19Kwa nini sasa sheria ilitolewa? Iliongezwa kwa sababu ya makosa, mpaka mzao wa Ibrahimu aje kwa wale ambao kwao alikuwa ameahidiwa. Sheria iliwekwa katika shinikizo kupitia malaika kwa mkono wa mpatanishi.
20Sasa mpatanishi humaanisha zaidi ya mtu mmoja, bali Mungu ni mmoja peke yake.
21Kwa hiyo je sheria iko kinyume na ahadi za Mungu? La hasha! Kwa kuwa kama sheria iliyokuwa imetolewa ilikuwa na uwezo wa kuleta uzima, haki ingepatikana kwa sheria.
22Lakini badala yake, andiko limefunga mambo yote chini ya dhambi. Mungu alifanya hivi ili kwamba ahadi yake ya kutuokoa sisi kwa imani katika Yesu Kristo iweze kupatikana kwa wale wanao amini.
23Lakini kabla ya imani katika Kristo haijaja, tulikuwa tumefungwa na kuwa chini ya sheria hadi uje ufunuo wa imani.
24Kwa hiyo sheria ilifanyika kiongozi wetu hadi Kristo alipokuja, ili kwamba tuhesabiwe haki kwa imani.
25Sasa kwa kuwa imani imekuja, hatuko tena chini ya mwangalizi.
26Kwa kuwa ninyi nyote ni watoto wa Mungu kupitia imani katika Kristo Yesu.
27Wote ambao mlibatizwa katika Kristo mmejivika Kristo.
28Hakuna Myahudi wala Myunani, mtumwa wala huru, mwanaume wala mwanamke, kwa kuwa ninyi nyote ni mmoja katika Kristo Yesu.
29Kama ninyi ni wa Kristo, basi ni uzao wa Ibrahimu, warithi kwa mujibu wa ahadi.