Text copied!
CopyCompare
Biblia ya Kiswahili - Wagalatia

Wagalatia 1

Help us?
Click on verse(s) to share them!
1Mimi ni Paulo mtume. Mimi sio mtume kutoka kwa wanadamu wala kupitia kwa mwanadamu, lakini kupitia kwa Yesu Kristo na Mungu Baba aliyemfufua kutoka kwa wafu.
2Pamoja na ndugu wote na mimi, ninayaandikia makanisa ya Galatia.
3Neema iwe kwenu na amani itokayo kwa Mungu Baba yetu na Bwana Yesu Kristo,
4aliyejitoa mwenyewe kwa ajili ya dhambi zetu ili kwamba atukomboe na nyakati hizi za uovu, kutokana na mapenzi ya Mungu wetu na Baba.
5Kwake uwe utukufu milele na milele.
6Ninashangaa kwamba mnageukia haraka kwenye injili nyingine. Ninashangaa kwamba mnageukia mbali kutoka kwake yeye aliyewaita kwa neema ya Kristo.
7Hakuna injili nyingine, lakini kuna baadhi ya watu wanao wasababishieni nyinyi matatizo na kutaka kubadilisha injili ya Kristo.
8Lakini hata kama ni sisi au malaika kutoka mbinguni atatangaza kwenu injili tofauti na ile tuliyoitangaza kwenu, na alaaniwe.
9Kama tulivyo sema mwanzoni, na sasa nasema tena, “Kama kuna mtu atawatangazia kwenu injili tofauti na mliyoipokea, na alaaniwe.”
10Kwani sasa hivi ninatafuta uthibitisho wa watu au Mungu? Ninatafuta kuwafurahisha wanadamu? Kama ninaendelea kujaribu kuwafurahisha wanadamu, mimi sio mtumishi wa Kristo.
11Ndugu, ninataka ninyi mjue kwamba injili niliyoitangaza haitokani na wanadamu.
12Sikuipokea kutoka kwa mtu, wala sikufundishwa. Badala yake, ilikuwa ni kwa ufunuo wa Yesu Kristo kwangu.
13Mmekwisha sikia juu ya maisha yangu ya nyuma katika dini ya Kiyahudi, jinsi nilivyokuwa nikilitesa kwa ukali kanisa la Mungu zaidi ya kipimo na kuliteketeza.
14Nilikuwa nimeendelea katika Dini ya Kiyahudi zaidi ya ndugu zangu wengi Wayahudi. Nilikuwa na bidii sana katika tamaduni za baba zangu.
15Lakini Mungu alipendezwa kunichagua mimi kutoka tumboni mwa mama. Aliniita mimi kupitia neema yake
16kumdhihirisha Mwanawe ndani yangu, ili kwamba nimtangaze yeye miongoni mwa watu wa mataifa. Wala sikutafuta ushauri wa mwili na damu
17na sikupanda kwenda Yerusalem kwa wale waliokuwa mitume kabla yangu. Badala yake nilienda Uarabuni na baadae kurudi Damesiki.
18Kisha baada ya miaka mitatu nilipanda kwenda Yerusalemu kumtembelea Kefa, nikakaa naye kwa siku kumi na tano.

19Lakini sikuona mitume wengine isipokuwa Yakobo, ndungu yake na Bwana.
20Tazama, mbele za Mungu, sidanganyi kwa kile niandikacho kwenu.
21Kisha nilikwenda mikoa ya Shamu na Kilikia.
22Sikuwa najulikana kwa macho kwa makanisa ya Uyahudi yale yaliyokuwa katika Kristo,
23lakini walikuwa wakisikia tu, “Yeye aliyekuwa akitutesa sasa anatangaza imani aliyokuwa akiiharibu.”
24Walikuwa wakimtukuza Mungu kwa ajili yangu.