Text copied!
CopyCompare
Biblia ya Kiswahili - Luka - Luka 15

Luka 15:16-23

Help us?
Click on verse(s) to share them!
16Na akawa akitamani kujishibisha kwa maganda waliyokula nguruwe kwa sababu hakuna mtu aliempa kitu chochote apate kula.
17Ila yule mwana mdogo alipozingatia moyoni mwake, alisema 'ni watumishi wangapi wa baba yangu wanachakula kingi cha kutosha na mimi niko hapa, ninakufa na njaa!
18Nitaondoka na kwenda kwa baba yangu, na kumwambia, “Baba nimekosa juu ya mbingu na mbele ya macho yako.
19Sistahili kuitwa mwana wako tena; nifanye kama mmoja wa watumishi wako.”
20Ndipo akaondoka akaenda kwa baba yake. Alipokua angali mbali baba yake alimuona akamwonea huruma akaenda mbio na kumkumbatia na kumbusu.
21Yule mwana akamwambia, 'baba nimekosa juu ya mbingu na mbele ya macho yako sistahili kuitwa mwana wako.'
22Yule baba aliwaambia watumishi wake, 'lileteni upesi vazi lililo bora, mkamvike mtieni na pete kidoleni na viatu miguuni.
23Kisha mleteni ndama yule alienona mkamchinje tule na kufurai.

Read Luka 15Luka 15
Compare Luka 15:16-23Luka 15:16-23