Text copied!
CopyCompare
Biblia ya Kiswahili - Hesabu - Hesabu 22

Hesabu 22:25-29

Help us?
Click on verse(s) to share them!
25Yule punda akamwona yule malaika wa BWANA tena. Akasogea zaidi ukutani na kuubana mguu wa Balaamu ukutani. Balaamu akampiga tena yule punda.
26Yule malaika wa BWANA akasogea mbele zaidi kwenye eneo jingine jembamba zaidi ambalo haikuwezekana kugeuka upande mwingine.
27Yule Punda akamwona tena yule malaika wa BWANA, akalala chini ya Balaamu. Hasira za Balaamu zikawaka, akampiga yule punda kwa fimbo yake.
28Kisha BWANA akafungua kinywa cha punda na akaongea. Akamwambia Balaamu, “Nimekukosea nini kiasi kwamba umenipiga mara tatu?”
29Balaamu akamjibu yule punda, “Ni kwa sababu umenitendea kwa ujinga. Natamani kama ningekuwa na upanga mkononi mwangu, kama ningekuwa nao, sasa hivi ningekuwa nimekuua.”

Read Hesabu 22Hesabu 22
Compare Hesabu 22:25-29Hesabu 22:25-29