Text copied!
CopyCompare
Biblia ya Kiswahili - 1Wafalme - 1Wafalme 16

1Wafalme 16:4-17

Help us?
Click on verse(s) to share them!
4Mbwa watamla yeyote ambaye anatoka kwa Baasha wanaofia mjini, na ndege wa angani watamla yeyote anayaefia shambani.”
5Lakini kwa mambo mengine yanayohusiana na Baasha, aliyofanya, na uwezo wake, je, hayakuandikwa katika kitabu cha matukio ya wafalme wa Israeli?
6Baasha akalala na mababu zake na akazikwa Tirza, na Ela mwanae akawa mfalme mahali pake.
7Kwa kupitia nabii Yehu mwana wa Hanani neno la BWANA likaja kinyume na Baasha na familia yake, wote kwa sababu ya maovu yote aliyofanya machoni pa BWANA, akamghadhabisha kwa kazi ya mikono yake, kama familia ya Yeroboamu, na kwa sababu alikuwa ameiua familia yote ya Yeroboamu.
8Katika mwaka wa kumi na sita wa Asa mfalme wa Yuda, Ela mwana wa Baasha akaanza kutawala juu ya Israeli kule Tirza; akatawala kwa miaka miwili.
9Mtumishi wake Zimri, mkuu wa nusu ya magari yake akatengeneza hila dhidi yake. Wakati huo Ela alikuwa Tirza, akinywa na kulewa kwenye nyumba ya Arza, ambaye alikuwa mkuu wa watumishi wa nyumbani huko Tirza.
10Zimri akaiingia ndani, akamshambulia na kumwua, katika mwaka wa ishirini na saba wa Asa mfalme wa Yuda, naye akawa mfalme mahali pake.
11Zimri alipoaanza kutawala, mara tu baada ya kukaa kwenye kiti cha enzi, akawaua wanafamilia wote wa Baasha. Hakumwacha mtoto hata mmoja wa kiume, hakuna hata wa ndugu yake wala wa rafiki zake.
12Kwa hiyo Zimri aliingamiza familia yote ya Baasha, kama alivyokuwa ameambiwa kwa neno la BWANA, ambalo lilinenwa kinyume na Baasha na nabii Yehu,
13kwa dhambi zote za Baasha na za Ela mwanae ambazo walizifanya, ambazo kwazo waliisababisha Israeli kufanya dhambi, kiasi c ha kumghadhabisha BWANA, Mungu wa Israeli, kuzikasilikia sanamu zao.
14Kwa mambo mengine yanayohusiana na Ela, yote ambayo alifanya, je hayajaandikwa kwenye kitabu cha matukio ya wafalme wa Israeli?
15Katika mwaka wa ishirini na saba wa Asa mfalme wa Yuda, Zimri alitawala kwa siku saba tu kule Tirza. Jeshi likafanya kambi kule Gibethoni, ambao ni mji wa Wafilisti.
16Lile jeshi lililokuwa limeweka kambi kule lilisikika lilksema, “Zimri amepanga njama na amemwua mfalme.” Kwa hiyo siku hiyo hapo kambini, Israeli yote ikamtangaza Omri, mkuu wa jeshi, kuwa mfalme wa Israeli.
17Omri akapanda kutoka Gibethoni na Israeli yote pamoja naye, nao wakauhusuru Tirza.

Read 1Wafalme 161Wafalme 16
Compare 1Wafalme 16:4-171Wafalme 16:4-17