Text copied!
Bibles in Swahili (individual language)

1Wafalme 16:4-17 in Swahili (individual language)

Help us?

1Wafalme 16:4-17 in Biblia ya Kiswahili

4 Mbwa watamla yeyote ambaye anatoka kwa Baasha wanaofia mjini, na ndege wa angani watamla yeyote anayaefia shambani.”
5 Lakini kwa mambo mengine yanayohusiana na Baasha, aliyofanya, na uwezo wake, je, hayakuandikwa katika kitabu cha matukio ya wafalme wa Israeli?
6 Baasha akalala na mababu zake na akazikwa Tirza, na Ela mwanae akawa mfalme mahali pake.
7 Kwa kupitia nabii Yehu mwana wa Hanani neno la BWANA likaja kinyume na Baasha na familia yake, wote kwa sababu ya maovu yote aliyofanya machoni pa BWANA, akamghadhabisha kwa kazi ya mikono yake, kama familia ya Yeroboamu, na kwa sababu alikuwa ameiua familia yote ya Yeroboamu.
8 Katika mwaka wa kumi na sita wa Asa mfalme wa Yuda, Ela mwana wa Baasha akaanza kutawala juu ya Israeli kule Tirza; akatawala kwa miaka miwili.
9 Mtumishi wake Zimri, mkuu wa nusu ya magari yake akatengeneza hila dhidi yake. Wakati huo Ela alikuwa Tirza, akinywa na kulewa kwenye nyumba ya Arza, ambaye alikuwa mkuu wa watumishi wa nyumbani huko Tirza.
10 Zimri akaiingia ndani, akamshambulia na kumwua, katika mwaka wa ishirini na saba wa Asa mfalme wa Yuda, naye akawa mfalme mahali pake.
11 Zimri alipoaanza kutawala, mara tu baada ya kukaa kwenye kiti cha enzi, akawaua wanafamilia wote wa Baasha. Hakumwacha mtoto hata mmoja wa kiume, hakuna hata wa ndugu yake wala wa rafiki zake.
12 Kwa hiyo Zimri aliingamiza familia yote ya Baasha, kama alivyokuwa ameambiwa kwa neno la BWANA, ambalo lilinenwa kinyume na Baasha na nabii Yehu,
13 kwa dhambi zote za Baasha na za Ela mwanae ambazo walizifanya, ambazo kwazo waliisababisha Israeli kufanya dhambi, kiasi c ha kumghadhabisha BWANA, Mungu wa Israeli, kuzikasilikia sanamu zao.
14 Kwa mambo mengine yanayohusiana na Ela, yote ambayo alifanya, je hayajaandikwa kwenye kitabu cha matukio ya wafalme wa Israeli?
15 Katika mwaka wa ishirini na saba wa Asa mfalme wa Yuda, Zimri alitawala kwa siku saba tu kule Tirza. Jeshi likafanya kambi kule Gibethoni, ambao ni mji wa Wafilisti.
16 Lile jeshi lililokuwa limeweka kambi kule lilisikika lilksema, “Zimri amepanga njama na amemwua mfalme.” Kwa hiyo siku hiyo hapo kambini, Israeli yote ikamtangaza Omri, mkuu wa jeshi, kuwa mfalme wa Israeli.
17 Omri akapanda kutoka Gibethoni na Israeli yote pamoja naye, nao wakauhusuru Tirza.
1Wafalme 16 in Biblia ya Kiswahili