Text copied!
CopyCompare
Biblia ya Kiswahili - Yoshua - Yoshua 18

Yoshua 18:14-23

Help us?
Click on verse(s) to share them!
14Kisha mpaka ukaendelea upande mwingine: katika upande wa magharibi uligeukia upande wa kusini, ulienda mbele kuukabili mlima ulio ng'ambo ya Bethi Horoni. Mpaka huu ulikomea huko Kiriathi Baali (ambao ndio Kiriathi Yearimu), mji ambao ulikuwa ni wa kabila la Yuda. Na huu ndio ulikuwa ni mpaka katika upande wa magharibi.
15Katika upande wa kusini, mpaka ulianzia nje tu ya Kiriathi Yearimu. Mpaka uliendelea kutoka Efroni hata chemichemi ya maji ya Neftoa.
16Kisha mpaka ulishuka chini hadi mpaka wa mlima ambao ulikuwa mkabala ya bonde la Beni Hinomu, ambalo lililokuwa katika upande wa kaskazini mwishoni mwa bonde la Refaimu. Kisha ulishuka chini kuelekea bonde la Hinomu, sehemu ya kusini mwa mteremko wa Wayebusi, na uliendelea kushuka chini hadi Eni Rogeli.
17Ulizunguka upande wa kaskazini, kuelekea mwelekeo wa Eni Shemeshi, na kutoka hapa ulienda hadi Gelilothi, ambao ulikuwa mkabala na mwinuko wa Adumimu. Kisha ulishuka chini kuelekea Jiwe la Bohani mwana wa Rubeni.
18Ulipita kuelekea upande wa kaskazini wa bega la Bethi Araba na chini kuelekea Araba.
19Mpaka ulipita hadi upande wa bega la kaskazini la Bethi Hogla. Mpaka ulikome katika ghuba ya kaskazini mwa Bahari ya Chumvi, katika upande wa kusini mwishoni mwa Yordani. Huu ulikuwa ni mpaka wa upande wa kusini.
20Yordani ulikuwa mpaka wake katika upande wa mashariki. Na huu ulikuwa ni urithi wa kabila la Benyamini, na walipewa kwa kila ukoo wao, mpaka baada ya mpaka, kwa kuizunguka nchi yote.
21Kwa hiyo sasa miji ya kabila la Benyamini kufuatana na koo zao ilikuwa ni Yeriko,
22Bethi Hogla, Emeki Kezizi, Bethi Araba, Zemaraimu, Betheli,
23Avimu, Para, Ofra,

Read Yoshua 18Yoshua 18
Compare Yoshua 18:14-23Yoshua 18:14-23