Text copied!
CopyCompare
Biblia ya Kiswahili - Luka - Luka 8

Luka 8:39-54

Help us?
Click on verse(s) to share them!
39“Rudi kwenye nyumba yako na uhesabu yale yote ambayo Mungu amekutendea” Huyu mtu aliondoka, akitangaza pote katika mji wote yale yote ambayo Yesu aliyofanya kwa ajili yake.
40Na Yesu akarudi, makutano wakamkaribisha, kwa sababu wote walikuwa wanamngoja.
41Tazama akaja mtu mmoja anaitwa Yairo ni mmoja kati ya viongozi katika sinagogi. Yairo akaanguka miguuni pa Yesu na kumsihi aende nyumbani kwake,
42kwa sababu alikuwa na mtoto msichana mmoja tu, mwenye umri wa miaka kumi na wibili, na alikuwa katika hali ya kufa. Na alipokuwa akienda, makutano walikuwa wakisongama dhidi yake.
43Mwanamke mwenye kutokwa damu kwa miaka kumi na miwili alikuwa pale na alitumia pesa zote kwa waganga, lakini hakuna aliyemponya hata mmoja,
44alikuja nyuma ya yesu na kugusa pindo la vazi lake, na ghafla kutokwa damu kukakoma.
45Yesu akasema, “Nani ambaye kanigusa?” Walipokataa wote, Petro akasema, Bwana Mkubwa, umati wa watu wanakusukuma na wanakusonga.”
46Lakini Yesu akasema, “Mtu mmoja alinigusa, maana nilijua nguvu zimetoka kwangu.”
47Mwanamke alipoona ya kuwa hawezi kuficha alichokifanya, akaanza kutetemeka, akaanguka chini mbele za Yesu alitangaza mbele ya watu wote sababu zilizofanya amguse na vile alivyoponywa gafla.
48Kisha akasema kwake, “Binti, imani yako imekufanya uwe mzima. Enenda kwa Amani.”
49Alipokuwa akiendelea kusema, mtu mmoja akaja kutoka kwenye nyumba ya kiongozi wa sinagogi, akisema, “Binti yako amefariki. Usimsumbue mwalimu.”
50Lakini Yesu aliposikia hivyo, alimjibu, “Usiogope. Amini tu, na ataokolewa.”
51Kisha alipoingia kwenye hiyo nyumba, hakuruhusu mtu yeyote kuingia pamoja naye, isipokuwa Petro, Yohana na Yakobo, baba yake binti, na mama yake.
52Sasa watu wote walikuwa wanaomboleza na kutoa sauti kwa ajili yake, lakini akasema, “Msipige kelele, hajafa, lakini amelala tu.”
53Lakini wakamcheka kwa dharau, wakijua kuwa amekufa.
54Lakini Yeye, akimshika binti mkono, akaita kwa sauti, akisema, “Mtoto, inuka”

Read Luka 8Luka 8
Compare Luka 8:39-54Luka 8:39-54