39 “Rudi kwenye nyumba yako na uhesabu yale yote ambayo Mungu amekutendea” Huyu mtu aliondoka, akitangaza pote katika mji wote yale yote ambayo Yesu aliyofanya kwa ajili yake.
40 Na Yesu akarudi, makutano wakamkaribisha, kwa sababu wote walikuwa wanamngoja.
41 Tazama akaja mtu mmoja anaitwa Yairo ni mmoja kati ya viongozi katika sinagogi. Yairo akaanguka miguuni pa Yesu na kumsihi aende nyumbani kwake,
42 kwa sababu alikuwa na mtoto msichana mmoja tu, mwenye umri wa miaka kumi na wibili, na alikuwa katika hali ya kufa. Na alipokuwa akienda, makutano walikuwa wakisongama dhidi yake.
43 Mwanamke mwenye kutokwa damu kwa miaka kumi na miwili alikuwa pale na alitumia pesa zote kwa waganga, lakini hakuna aliyemponya hata mmoja,
44 alikuja nyuma ya yesu na kugusa pindo la vazi lake, na ghafla kutokwa damu kukakoma.
45 Yesu akasema, “Nani ambaye kanigusa?” Walipokataa wote, Petro akasema, Bwana Mkubwa, umati wa watu wanakusukuma na wanakusonga.”
46 Lakini Yesu akasema, “Mtu mmoja alinigusa, maana nilijua nguvu zimetoka kwangu.”
47 Mwanamke alipoona ya kuwa hawezi kuficha alichokifanya, akaanza kutetemeka, akaanguka chini mbele za Yesu alitangaza mbele ya watu wote sababu zilizofanya amguse na vile alivyoponywa gafla.
48 Kisha akasema kwake, “Binti, imani yako imekufanya uwe mzima. Enenda kwa Amani.”
49 Alipokuwa akiendelea kusema, mtu mmoja akaja kutoka kwenye nyumba ya kiongozi wa sinagogi, akisema, “Binti yako amefariki. Usimsumbue mwalimu.”
50 Lakini Yesu aliposikia hivyo, alimjibu, “Usiogope. Amini tu, na ataokolewa.”
51 Kisha alipoingia kwenye hiyo nyumba, hakuruhusu mtu yeyote kuingia pamoja naye, isipokuwa Petro, Yohana na Yakobo, baba yake binti, na mama yake.
52 Sasa watu wote walikuwa wanaomboleza na kutoa sauti kwa ajili yake, lakini akasema, “Msipige kelele, hajafa, lakini amelala tu.”
53 Lakini wakamcheka kwa dharau, wakijua kuwa amekufa.
54 Lakini Yeye, akimshika binti mkono, akaita kwa sauti, akisema, “Mtoto, inuka”