Text copied!
CopyCompare
Biblia Takatifu - Luka - Luka 13

Luka 13:11-23

Help us?
Click on verse(s) to share them!
11Na hapo palikuwa na mwanamke mmoja aliyekuwa mgonjwa kwa miaka kumi na minane kutokana na pepo aliyekuwa amempagaa. Kwa sababu hiyo, mwili wake ulikuwa umepindika vibaya hata asiweze kusimama wima.
12Yesu alipomwona, alimwita, akamwambia, “Mama, umeponywa ugonjwa wako.”
13Akamwekea mikono, na mara mwili wake ukawa wima tena, akawa anamtukuza Mungu.
14Lakini mkuu wa sunagogi alikasirika kwa sababu Yesu alikuwa amemponya siku ya Sabato. Hivyo akawaambia wale watu walikusanyika pale, “Mnazo siku sita za kufanya kazi. Basi, fikeni siku hizo mkaponywe magonjwa yenu; lakini msije siku ya Sabato.”
15Hapo Bwana akamjibu, “Enyi wanafiki! Nani kati yenu hangemfungua ng'ombe au punda wake kutoka zizini ampeleke kunywa maji, hata kama siku hiyo ni ya Sabato?
16Sasa, hapa yupo binti wa Abrahamu ambaye Shetani alimfanya kilema kwa muda wa miaka kumi na minane. Je, haikuwa vizuri kumfungulia vifungo vyake siku ya Sabato?”
17Alipokwisha sema hayo, wapinzani wake waliona aibu lakini watu wengine wote wakajaa furaha kwa sababu ya mambo yote aliyotenda.
18Yesu akauliza: “Ufalme wa Mungu unafanana na nini? Nitaulinganisha na nini?
19NI kama mbegu ya haradali aliyotwaa mtu mmoja na kuipanda shambani mwake; ikaota hata ikawa mti. Ndege wa angani wakajenga viota vyao katika matawi yake.”
20Tena akauliza: “Nitaulinganisha Ufalme wa Mungu na nini?
21Ni kama chachu aliyoitwaa mama mmoja na kuichanganya pamoja na unga debe moja kisha unga wote ukaumuka wote.”
22Yesu alindelea na safari yake kwenda Yerusalemu huku akipitia mijini na vijijini, akihubiri.
23Mtu mmoja akamwuliza, “Je, Mwalimu, watu watakaookoka ni wachache?”

Read Luka 13Luka 13
Compare Luka 13:11-23Luka 13:11-23