Text copied!
CopyCompare
Biblia ya Kiswahili - Hesabu - Hesabu 26

Hesabu 26:1-14

Help us?
Click on verse(s) to share them!
1Ilitokea baada ya tauni ambayo BWANA alimwambia Musa na Eliazari mwana wa Haruni kuhani, Alisema,
2Wahesabu watu wote wa Israeli, kuanzia miaka ishirini na zaidi, kwa jamaa ya familia zao wote ambao wanaweza kwenda kwenye vita kwa ajili ya Israeli.”
3Kwa hiyo Musa na Eliazari kuhani wakawaambia katika uwanda wa Moabu karibu na Yorodani kule Yeriko na kusema,
4Wahesabuni watu, kuanzi umri wa miaka ishirini na zaidi kama BWANA alivyomwamuru Musa na watu wa Israeli walitoka katika nchi ya Misri.”
5Reubeni ndiye aliyekuwa wa kwanza, Kutoka kwa mwana wake Hanoki ulitokea ukoo wa Wahanoki. Kutoka kwa Palu ulitokea ukoo wa Wapalu.
6Kutoka Hezroni. ulitokea ukoo wa Wahezroni. Kutoka kwa Kami ulitokea ukoo wa Wakami.
7Hizi ndizo zilikuwa koo za uzao wa Reubeni, ambzo idadi yao ilikuwa wanaume 43, 730.
8Eliabu alikuwa mwana wa Palu.
9Wana wa Eliabu walikuwa ni Nemueli, Dathani. na Abiramu. Hawa ni walewale Dathani na Abiramu waliomfuata Kora waliompinga Musa na Haruni na kumpinga BWANA.
10Pale ambapo dunia ilifungua kinywa na kuwameza pamoja na Kora wakati ambapo wafuasi wa Kora walikufa. Wakati ule, moto uliteketeza wanaume 250, amboa wlikuwa ishara ya onyo.
11Lakini uzao wa Kora haukufa.
12Ukoo wa uzao wa Simeoni walikuwa hawa wafuatao: Kutoka kwa Nemueli, ukoo wa Wanemueli, kwa Jamini, ukoo wa Wajamini, kwa Jakini, ukoo wa Wajakini,
13kwa Zera, ukoo wa Wazera, kwa Shauli, ukoo wa Washauli.
14Hizi ndizo koo za uzao wa Simeoni, idadi yao ilikuwa wanaume 22, 200.

Read Hesabu 26Hesabu 26
Compare Hesabu 26:1-14Hesabu 26:1-14