Text copied!
CopyCompare
Biblia ya Kiswahili - Hesabu - Hesabu 22

Hesabu 22:35-39

Help us?
Click on verse(s) to share them!
35Lakini yule malaika wa BWANA akamwambia Balaamu, “endelea na wale watu. Lakini utasema maneno nitakayokwambia tu.” Kwa hiyo Balaamu akaendelea na wale vioingozi wa Balaki.
36Balaki aliposikia kuwa Balaamu alikuwa amekuja, alienda kukutana naye kule mjini Moabu pale Amoni, ambao uko mpakani.
37Balaki akamwambia Balaamu, “Je, mimi sikutuma watu kukuita? Basi kwa nini hukuja kwangu? Je, mimi sina uwezo wa kukufanya uheshimike?”
38Ndipo Balaamu alipomjibu Balaki, “Tazama, mimi nimekuja kwako. Je mimi sina mamlaka ya kusema chochote? Mimi ninaweza kusema maneno ambayo Mungu ameweka kinywani mwangu.”
39Balaamu akaenda na Balaki, na Wakafika Kiriathi Huzothi.

Read Hesabu 22Hesabu 22
Compare Hesabu 22:35-39Hesabu 22:35-39