Text copied!
CopyCompare
Biblia ya Kiswahili - Hesabu - Hesabu 17

Hesabu 17:1-11

Help us?
Click on verse(s) to share them!
1BWANA akanena na Musa, akasema,
2“Waambie wana wa Israeli wakuletee fimbo za kutembelea moja kwa kila jamaa, fimbo kumi na mbili. Uandika jina la kila mmoja kwenye hizo fimbo.
3Utaandika jina la Haruni kwenye jina la Lawi. Kutakuwa na fimbo moja kwa kila kiongozi kutoka kwenye kabila la mababu zake.
4Utaziweka hizo fimbo kwenye hema ya kukutania mbele ya amri za agano, ambapo Mimi hukutana na wewe. Itakuwa hivi,
5fimbo ya mtu yule ninayemchagua itachipua. Nitazuia watu wa Israeli walalamikao, ambao wanaongea kinyume na wewe.”
6Kwa hiyo Musa akawaambia wana wa Israeli. Viongozi wote wa kabila wakampatia fimbo, fimbo moja kutoka kwa kila kiongozi, aliyechaguliwa kutoka kwenye kila kabila ya babu zao, jumla yake fimbo kumi na mbili. Fimbo ya Haruni ilikuwa miongoni mwa fimbo hizo.
7Ndipo Musa alipoziweka zile fimbo mbele ya BWANA katika hema ya amri ya agano.
8Siku iliyofuata Musa aliingia kwenye hema ya amri ya agano, na tazama, fimbo ya Haruni kwa ajili ya Kabila la Lawi ilikuwa imetoa machipukizi. Machipukizi yalikuwa hadi kuchanua maua na kuzaa malozi mabivu!
9Musa akazitoa fimbo zote kutoka kwa BWANA kwa watu wote wa Israeli, na kila mtu akachukua fimbo yake.
10BWANA akamwambua Musa, “Iweke fimbo ya Haruni mbele ya amri za agano. Iweke iwe ishara ya hatia mbele ya watu waliopinga ili ukomeshe malalamiko dhidi yangu, vinginevyo watakufa.”
11Musa akafanya kama BWANA alivyoagiza.

Read Hesabu 17Hesabu 17
Compare Hesabu 17:1-11Hesabu 17:1-11