Text copied!
CopyCompare
Biblia ya Kiswahili - Ezra

Ezra 6

Help us?
Click on verse(s) to share them!
1Na mfalme dario akaamuru uchunguzi ufanyike katika nyumba ya kumbukumbu Babeli.
2Na katika mji wa Akmetha huko media chuo kilionekana: Kumbukumbu yake ilisema:
3“Katika mwaka wa kwanza mfalme Koresh, Koreshi alitoa amri kuhusu nyumba ya Mungu Yerusalem: 'Na nyumba ijengwe iwe sehemu ya kutoa dhabihu, misingi yake iwekwe, urefu wake uwe sitini,
4na upana wake uwe sitini, sehemu tatu za mawe makubwa na sehemu moja ya mbao mpya, na gharama hizo zitalipwa kutoka nyumba ya mfalme.
5Sasa vilirudishwe tena vitu vya dhahabu na fedha vilivyokuwa kwenye nyumba ya Mungu ambavyo Nebukadineza alivichukua kuvipeleka Babeli kutoka kwenye Hekalu Yerusalem. Na avirudishe tena Yerusalem Hekaluni. Na utaviweka tena kwenye nyumba ya Mungu.
6Sasa Tetanai, mkuu wa jimbo ngambo ya mto, Shethar - Bozenai na wenzao walio katika mji ngambo ya mto, wakajitenga,
7wakaacha kazi ya nyumba ya Mungu pekee. Viongozi na wazee wa kiyahudi watajenga nyumba ya Mungu mahali pake.
8Ninatoa agizo kwamba lazima lifanyike kwa wazee wa kiyahudi wanaojenga nyumba ya Mungu: Mchango kutoka kwa mfalme ushuru ngambo ya mto, utatumika katika kuwalipa watu hawa ili kwamba kazi yao isiweze kusimama.
9Chochote kitakachohitajika, ngombe wachanga, kondoo au kondoo wa sadaka ya kutekezwa kwa ajili ya Mungu wa mbinguni, ngano, chumvi, divai na mafuta kadri ya maagizo ya makuhani wa Yerusalem - wapatie vitu hivi kila siku bila kikomo.
10fanya hivyo ili kwamba wataleta sadaka kwa Mungu wa mbinguni na wataomba kwa ajili yangu mfalme na watoto wangu.
11Mimi nina agiza kwamba yeyote atakayevunja amri hii, Chuma kitolewe katika nyumba yake. Na awekwe juu yake. Na nyumba yake itabadilishwa kuwa takataka kwa sababu hii.
12Mungu huyu aliyesababisha jina lake kuwepo atamwondoa mfalme au mtu atakayebadili agizo hili au kuondosha nyumba ya Mungu katika Yerusalem. Mimi Dario nimeagiza hili, lifanyike kwa makini.
13Na kwa sababu ya amri iliyotumwa na mfalme Dario, Tatenai kiongozi mji ngambo ya mto na Sheshthar -Bozenai na wenzao. wakafanya kila kitu kama Mfalme Dario alivyoagiza.
14Hivyo wazee wa kiyahudi wakajenga kama Hagai na Zakaria walivyoelekeza kwa kutabiri. Wakajenga kama amri ilivyotolewa na Mungu wa Israel na Koreshi, Dario na Artashasta mfalme wa Uajemi.
15Nyumba ikakamilika siku ya tatu ya mwezi wa adari, katika mwaka wa sita wa kutawala mfalme Dario.
16watu wa Israel, makuhani, walawi na watu waliobaki wa uhamisho wakasheherekea kuweka wakfu nyumba ya Mungu kwa furaha.
17Wakatoa ngombe mia moja, kondoo mia moja na kondoo wengine mia nne kwa ajili ya kuweka wakfu nyumba ya Mungu. Mbuzi wa kiume kumi na wawili walitolewa kama sadaka ya dhambi kwa ajili ya waisrael wote kila kabila katika Israel.
18Pia wakawapa wajibu makuhani na walawi kufanya mgawanyo wa kazi ya Mungu katika Yerusalem. Kama ilivyoandikwa katika kitabu cha Musa.

19Hivyo wale waliokuwa utumwani wakasherehekea pasaka siku ya kumi na nne ya mwezi wa kwanza.
20Makuhani na walawi wakajitakasa wenyewe na wakachinja pasaka ya sadaka kwa ajili ya waliokuwa mateka wakiwemo na wao wenyewe.
21watu wa Israel ambao walikula nyama ya Pasaka ni wale waliorudi kutoka uhamishoni na walikuwa wamejitenga wenyewe kutoka kwa watu wasio safi wa nchi ile na kumchagua Yahwe, Mungu wa Israel.
22Walifurahi na kushangilia siku kuu ya mikate isiyochacha kwa siku saba, kwa sababu Yahwe amewarejeshea furaha na ameugeuza moyo wa mfalme wa Ashuru, na kuwatia nguvu kwa kazi ya nyumba, nyumba ya Mungu wa Israel.