Text copied!
CopyCompare
Biblia ya Kiswahili - 1Wafalme - 1Wafalme 8

1Wafalme 8:1-46

Help us?
Click on verse(s) to share them!
1Kisha Sulemani akawakusanya wazee wa Israeli, wakuu wote wa makabila, na viongozi wa familia za wana wa Israeli, mbele yake kuleYerusalemu, ili waliingize ndani lile sanduku la agano la BWANA kutoka mji wa Daudi, ambao ni Sayuni.
2Wanaume wote wa Israeli walikusanyika mbele ya mfalme Sulemani kwenye sherehe, katika mwezi wa Ethanim, ambao ndio mwezi wa saba.
3Wazee wote wa Israeli walikuja, na makuhani wakalibeba lile sanduku.
4Wakalileta lile sanduku la BWANA, lIle hema la kukutania na mapambo yote matakatifu ambayo yalikuwa kwenye hema. Makuhani na Walawi wakavileta vitu hivi.
5Mfame Sulemani na mkutano wote wa Israeli wakaja pamoja mbele ya sanduku, wakatoa sadaka za kondoo na makisai ambazo hazikuweza kuhasabika.
6Makuhani wakalingiza ndani lile sanduku la agano la BWANA na wakaliweka mahali pake, ndani ya chumba cha ndani, patakatifu sana, chini ya yale mabawa ya makerubi.
7Kwa kuwa makerubi walitandaza mabawa yao hadi mahali pa sanduku la agano, na walifunika sanduku na miti yake kwani ilitumika kulibeba.
8Ile miti ilikuwa mirefu sana kiasi kwamba miishio yake ilionekana tokea kwenye eneo takatifu mbele ya chumba cha ndani, lakini haikuweza kuonekana kutokea nje. Miti hiyo iko mpaka leo.
9Ndani ya sanduku hapakuwemo na kitu chochote isipokuwa vile vidonge vya mawe ambavyo Musa aliviweka alipokuwa mlima Horebu, wakati BWANA alipofanya agano na watu wa Israeli walipotoka kwenye nchi ya Misri.
10Ilitokea kwamba wakati makuhani walipotoka mahali patakatifu, lile wingu lilifunika hekalu la BWANA.
11Makuhani hawakuweza kusimama kwa ajili ya kutumika kwa sababu utukufu wa BWANA ulifunika hekalu.
12Kisha Sulemani akasema, “BWANA amsema kuwa anaweza kuishi hata kwenye giza nene,
13Lakinni nimekujengea makao ya kujivunia, mahali pako pa kuishi milele.”
14Kisha mfalme akageuka na kuwabariki mkusanyiko wa watu wa Israeli, wakati huo mkusanyiko wa Waisraeli walikuwa wamesimama.
15Akasema, “BWANA, Mungu wa Israeli, asifiwe, ambaye alisema na baba yangu Daudi, na ametimiza kwa mikono yake, akisema,
16'Tangu siku ile niliyowatoa watu wangu Israeli kutoka Misri, sikuchagua mji wowote toka kwa makabila yote ya Israeli ambako ningeijenga nyumba, kwa ajili ya jina langu kuwemo humo. Hata hivyo, nilimchagua Daudi kuwatawala watu wangu Israeli.
17Sasa ilikuwa kwenye moyo wa Daudi baba yangu kujenga nyumba kwa jina la BWANA, Mungu wa Israeli.
18Lakini BWANA alimwambia baba yangu Daudi, 'Ilikuwa ndani ya moyo wako kunijengea nyumba kwa jina langu, ulifanya vyema kwa hilo kuwa ndani ya moyo wako.
19Ingawa hutanijengea nyumba; badala yake mwanao, mmoja wa wanao atakayezaliwa toka viunoni mwako, atanijengea nyumba kwa jina langu,'
20BWANA amelibeba lile neno slilokuwa amesema, kwa kuwa nimeinuka mahali pa baba yangu Daudi, na nimeketi kwenye kiti cha enzi cha Israeli, kama BWANA alivyoahidi. Nimeijenga nyumba kwa jina la BWANA, Mungu wa Israeli.
21Nimetengeneza mahali kwa ajili ya sanduku ndani yake, ambamo ndani yake kuna agano la BWANA, ambalo alifanya na baba zetu alipowatoa toka nchi ya Misri,”
22Sulemani alisimama mbele ya madhabahu ya BWANA, mbela ya mkusanyiko wote wa Waisraeli, naye akanyosha mikono yake kuelekea mbinguni.
23Akasema, “BWANA, Mungu wa Israeli, hakuna Mungu kama wewe juu mbinguni au chini duniani, ambaye hutunza agano lake kwa uaminifu kwa watumishi wako ambao hutembea mbele yako kwa mioyo yao yote;
24wewe ambaye umetunza ahadi yako na mtumishi wako Daudi baba yangu ile uliyomwahidi. Naam, ulisema kwa kinywa chako na sasa umeitimiza kwa mkono wako, kama ilivyo leo.
25Sasa basi, BWANA, Mungu wa Israeli, timiza kile ulichomwahidi mtumishi wako Daudi baba yangu, pale uliposema, 'Hautashindwa kunipa mtu mbele ya macho yangu ambaye ataketi katika kiti cha enzi cha Israeli, kama tu uzao wako watakuwa waangalifu kutembea mbele yangu, kama vile wewe ulivyotembea mbele yangu.'
26Sasa basi, Mungu wa Israeli, Ninaomba kwamba ile ahadi uliyofanya kwa mtumishi wako Daudi baba yangu, itimie.
27Je, ni kweli kwamba Mungu ataishi duniani? Tazama, Ulimwengu wote na mbingu hazikutoshi - sembuse nyumba hii niliyoijenga!
28Kwa hiyo Mungu naomba uyajali maombi haya ya mtumishi wako na maombi yake, BWANA, Mungu wangu; sikiliza kilio na maombi ambayo mtumishi wako anakuomba leo.
29Naomba ulitazame hekalu hili mchana na usiku, mahali ambapo ulisema, 'Jina langu na uwepo wangu utakuwa' - ili niweze kuwa nasikiliza maombi ambayo mtumishi wako ataomba mahali hapa.
30Kwa hiyo sikia maombi ya mtumishi wako na ya watu wako Israeli tunapokuwa tunaomba mahali hapa. Ndiyo, sikia kutokea mahali ambapo unaishi, kutoka katika mbingu za mbingu; na unaposikia tafadhali samehe.
31Kama mtu atamtendea uovu jirani yake na anapewa sharti la kiapo, na kama atakuja na kuapa mbele ya madhabahu yako katika nyumba hii,
32basi usikie kutoka mbinguni ukatende na kuwahukumu watumishi wako, ukamhukumu mwovu, ili kuwaletea tabia zake kichwani mwake, na kumtunza mwenye haki kuwa hana hatia, na kumpa thawabu yake ya haki.
33Watu wako Israeli watakapopigwa na adui kwa sabau ya kutenda dhambi dhidi yako, na kama watakurudia, na kulikiri jina lako, na kukusihi, na kuomba msamaha kwako katika hekalu hili-
34tafadhali nakuomba usikie kutoka mbinguni na usamehe dhambi za watu wako Israeli; uwarudishe katika nchi ambayo uliwapa mababu zao.
35Kama mbingu zitafungwa na mvua hazinyeshi kwa sababu watu wamekutenda dhambi wewe - na kama wataomba mahali hapa, na kulikiri jina lako, na kugeuka toka dhambi zao na kama umewapiga -
36basi sikia tokea mbinguni na usamehe dhambi za watumishi wako na za watu wako Israeli, utakapowafundisha njia njema inayowapasa; basi uinyeshee mvua nchi yako, ambayo uliwapa watu wako kuwa urithi.
37Na kama kuna njaa katika nchi, au kama kuna magonjwa, au ukungu, nzige au funza; au kama adui atavamia malango ya mji katika nchi yao, kama kuna tauni au magonjwa yeyote -
38na kama kuna mtu au wata wa Israeli wataomba - kila mmoja akaijua hiyo tauni katika moyo wake wakati akinyosha mikono yake katika hekalu hili.
39Basi usikie kutoka mbinguni, mahali unapoishi, utende na kusamehe, na umpe kila mtu thawabu anayostahili kwa kile anachofanya; wewe unajua moyo wake, kwa sababu ni wewe pekee yako ujuaye mioyo ya watu.
40Fanya hivi ili kwamba wawe na hofu kwako katika siku zote za maisha yao wanayoishi katika nchi uliyowapa mababu zetu.
41Na nyongeza yake, kuhusiana na mgeni ambaye si mtu wako wa Israeli: atakapokuja kutokea nchi ya mbali kwa sababu ya jina lako -
42kwa sababu watasikia jina lako lilivyo kuu, mkono wako wenye nguvu, na mkono wako ulioinuliwa - atakapokuja na kuomba mahali hapa pa hekalu,
43tafadhali usikie kutokea katika mbingu, mahali unapoishi, na umfanyie huyo mgeni akuombacho. Fanya hivi ili makundi ya wtu wote duniani wakujue jina lako na kukuhofia, kama wanavyofanya watu Israeli. Fanya hivyo ili wajue kwamba nyumba hii niliyoijenga inaitwa kwa jina lako.
44Na kama watu wko wataenda vitani dhidi ya adui, kwa njia yeyote unayoweza kuwatuma, na kama watakuomba wewe, BWANA, kuelekea mji huu uliuchagua, na kuekea nyumba ambayo nimeijenga kwa jina lako.
45Basi sikia tokea mbinguni maombi yao, dua zao, na uwasaidie wanachohitaji.
46Na kama watafanya dhambi dhidi yako, kwa kuwa hakuna hata mtu mmoja asiyefanya dhambi, na kama una hasira dhidi yao na kuwapeleka kwa maadui, ili kwamba maadui wawachukue mateka katika nchi yao, mbali au karibu.

Read 1Wafalme 81Wafalme 8
Compare 1Wafalme 8:1-461Wafalme 8:1-46