13Inuka! Waweke watu wakfu kwangu, na uwaambie, 'Jiwekeeni wakfu ninyi wenyewe kesho. Kwa kuwa, Yahweh, Mungu wa Israeli asema hivi, “Kuna vitu vilitengwa ili kuteketezwa ambavyo bado viko miongoni mwenu, Israeli. Hamtaweza kusimama mbele ya maadui zenu mpaka pale mtakapoviondoa miongoni mwenu vitu vyote ambavyo vilitengwa kwa ajili ya kuteketezwa.”
14Asubuhi, mtajisogeza wenyewe kwa makabila. Kabila lile ambalo Yahweh atalichagua litasogea karibu kwa koo zake. Ukoo ule ambao Yahweh atauchagua lazima usogee karibu kwa nyumba. Nyumba ambayo Yahweh ataichagua lazima isogee karibu kwa mtu mmoja mmoja.