Text copied!
CopyCompare
Biblia ya Kiswahili - Yoshua - Yoshua 21

Yoshua 21:19-34

Help us?
Click on verse(s) to share them!
19Miji waliyopewa makuhani, wana wa Haruni, ilikuwa ni miji kumi na mitatu kwa ujumla, kujumlisha na maeneo yake ya malisho.
20Na kwa ajili ya sehemu ya familia ya Kohathi iliyosalia, wale Walawi walio wa familia ya Kohathi, walipewa miji kutoka katika kabila la Efraimu kwa kupiga kura.
21Walipewa Shekemu pamoja na maeneo yake ya malisho katika nchi ya milima ya Efraimu - mji wa makimbilio kwa mtu aliyeua mtu bila kukusudia, na Gezeri pamoja na maeneo yake ya malisho,
22na Kibzaimu pamoja na maeneo yake ya malisho, na Bethi Horoni pamoja na maeneo yake ya malisho, ilikuwa miji minne kwa ujumla wake.
23Kutoka katika kabila la Dani, ukoo wa Kohathi ulipewa Elteke pamoja na maeneo yake ya malisho, na Gibethoni pamoja na maeneo yake ya malisho, na
24Aijaloni pamoja na maeneo yake ya malisho, na Gathrimoni pamoja na maeneo yake ya malisho, ilikuwa ni miji minne kwa ujumla wake.
25Kutoka katika nusu ya kabila la Manase, ukoo wa Kohathi walipewa miji miwili - Taanaki pamoja na maeneo yake ya malisho na Gathirimoni pamoja na maeneo yake ya malisho.
26Kulikuwa na miji kumi kwa ujumla wake kwa ajili ya koo zilizosalia za Wakohathi, pamoja na maeneo yao ya malisho.
27Kutoka katika nusu ya kabila la Manase, jamaa za Gershoni, ambazo hizi zilikuwa ni koo zingine za Walawi, zilipewa Golani katika Bashani pamoja na maeneo yao ya malisho, ni mji wa makimbilio kwa ajili ya mtu yeyote aliyeua mtu bila kukusudia, sambamba na Beeshitera pamoja na maeneo yake ya malisho - ilikuwa miji miwili kwa ujumla.
28Koo za Gershoni zilipewa pia miji minne kutoka kwa kabila la Isakari - Kishoni sambamba na maeneo yake ya malisho, Daberathi pamoja na maeneo yake ya malisho,
29Yarmuthi pamoja na maeneo yake ya malisho, na Engnimu pamoja na maeneo yake ya malisho.
30Kutoka katika kabila la Asheri, walipewa miji minne kwa ujumla - Mishali pamoja na maeneo yake ya malisho, Abdoni pamoja na maeneo yake ya malisho,
31Helikathi pamoja na maeneo yake ya malisho, na Rehobu pamoja na maeneo yake ya malisho.
32Kutoka kwa kabila la Nafutali, nasaba za Gershoni walipewa miji mitatu kwa ujumla - Kedeshi katika Galilaya pamoja na maeneo yake ya malisho, ulikuwa ni mji wa makimbilio kwa mtu yeyote aliyeua mtu bila kukusudia; na Hamothidori pamoja na maeneo yake ya malisho, na Kartani pamoja na maeneo yake ya malisho.
33Kulikuwa na miji kumi na mitatu kwa ujumla, kujumuisha na maeneo yake ya malisho, kwa ajili ya koo za Gershoni.
34Na kwa Walawi waliosalia, koo za Merari waliokuwa wamepewa kutoka katika kabila la Zabuloni: Yokneamu pamoa na maeneo yake ya marisho, Karta pamoja na maeneo yake ya malisho,

Read Yoshua 21Yoshua 21
Compare Yoshua 21:19-34Yoshua 21:19-34