Text copied!
Bibles in Swahili (individual language)

Yoshua 21:19-34 in Swahili (individual language)

Help us?

Yoshua 21:19-34 in Biblia ya Kiswahili

19 Miji waliyopewa makuhani, wana wa Haruni, ilikuwa ni miji kumi na mitatu kwa ujumla, kujumlisha na maeneo yake ya malisho.
20 Na kwa ajili ya sehemu ya familia ya Kohathi iliyosalia, wale Walawi walio wa familia ya Kohathi, walipewa miji kutoka katika kabila la Efraimu kwa kupiga kura.
21 Walipewa Shekemu pamoja na maeneo yake ya malisho katika nchi ya milima ya Efraimu - mji wa makimbilio kwa mtu aliyeua mtu bila kukusudia, na Gezeri pamoja na maeneo yake ya malisho,
22 na Kibzaimu pamoja na maeneo yake ya malisho, na Bethi Horoni pamoja na maeneo yake ya malisho, ilikuwa miji minne kwa ujumla wake.
23 Kutoka katika kabila la Dani, ukoo wa Kohathi ulipewa Elteke pamoja na maeneo yake ya malisho, na Gibethoni pamoja na maeneo yake ya malisho, na
24 Aijaloni pamoja na maeneo yake ya malisho, na Gathrimoni pamoja na maeneo yake ya malisho, ilikuwa ni miji minne kwa ujumla wake.
25 Kutoka katika nusu ya kabila la Manase, ukoo wa Kohathi walipewa miji miwili - Taanaki pamoja na maeneo yake ya malisho na Gathirimoni pamoja na maeneo yake ya malisho.
26 Kulikuwa na miji kumi kwa ujumla wake kwa ajili ya koo zilizosalia za Wakohathi, pamoja na maeneo yao ya malisho.
27 Kutoka katika nusu ya kabila la Manase, jamaa za Gershoni, ambazo hizi zilikuwa ni koo zingine za Walawi, zilipewa Golani katika Bashani pamoja na maeneo yao ya malisho, ni mji wa makimbilio kwa ajili ya mtu yeyote aliyeua mtu bila kukusudia, sambamba na Beeshitera pamoja na maeneo yake ya malisho - ilikuwa miji miwili kwa ujumla.
28 Koo za Gershoni zilipewa pia miji minne kutoka kwa kabila la Isakari - Kishoni sambamba na maeneo yake ya malisho, Daberathi pamoja na maeneo yake ya malisho,
29 Yarmuthi pamoja na maeneo yake ya malisho, na Engnimu pamoja na maeneo yake ya malisho.
30 Kutoka katika kabila la Asheri, walipewa miji minne kwa ujumla - Mishali pamoja na maeneo yake ya malisho, Abdoni pamoja na maeneo yake ya malisho,
31 Helikathi pamoja na maeneo yake ya malisho, na Rehobu pamoja na maeneo yake ya malisho.
32 Kutoka kwa kabila la Nafutali, nasaba za Gershoni walipewa miji mitatu kwa ujumla - Kedeshi katika Galilaya pamoja na maeneo yake ya malisho, ulikuwa ni mji wa makimbilio kwa mtu yeyote aliyeua mtu bila kukusudia; na Hamothidori pamoja na maeneo yake ya malisho, na Kartani pamoja na maeneo yake ya malisho.
33 Kulikuwa na miji kumi na mitatu kwa ujumla, kujumuisha na maeneo yake ya malisho, kwa ajili ya koo za Gershoni.
34 Na kwa Walawi waliosalia, koo za Merari waliokuwa wamepewa kutoka katika kabila la Zabuloni: Yokneamu pamoa na maeneo yake ya marisho, Karta pamoja na maeneo yake ya malisho,
Yoshua 21 in Biblia ya Kiswahili