Text copied!
CopyCompare
Biblia ya Kiswahili - Yoshua - Yoshua 13

Yoshua 13:10-22

Help us?
Click on verse(s) to share them!
10miji yote ya Sihoni, mfalme wa Waamori, ambaye alitawala katika Heshiboni, hata mpaka wa Waamori,
11Gileadi na mkoa wa Wageshuri na Maakathi, mlima wote wa Hermoni, Bashani yote mpaka Saleka;
12ufalme wote wa Ogu katika Bashani, aliyetawala katika Ashitarothi na Edrei - hawa ni wale waliosalia katika Refaimu - ambao Musa aliwapiga na kuwafukuzia mbali.
13Lakini watu wa Israeli hawakuwafukuza Wageshuri wala Wamakathi. Badala yake, Wageshuri na Wamakathi wanaishi miongoni mwa Waisraeli hadi leo.
14Kabila la Lawi pekee halikupewa urithi na Musa. Urithi wao ni sadaka za Yahweh, Mungu wa Israeli, zilizotolewa kwa moto, kama Mungu alivyomwagiza Musa.
15Musa aliwapa urithi kabila la Rubeni, ukoo kwa ukoo.
16Miliki yao ilikuwa kutoka Aroeri, juu ya ukingo wa bonde la Mto Arnoni, na mji ulio katikati ya bonde, na nyanda zote za Medeba.
17Wareubeni walipata pia Heshiboni, na miji yake yote zilizo katika uwanda, Diboni, na Bamathi Baali, na Bethi Baalimeoni,
18na Yahazi, na Kedemothi, na Mefaathi,
19na Kiriathaimu, na Sibuma, na Zerethishahari juu ya kilima cha bonde.
20Wareubeni walipata pia Bethi Peori, miteremko ya Pisiga, Bethi Yeshimothi,
21miji yote ya uwanda, na ufalme wote wa Sihoni, mfalme wa Waamori, ambaye alikuwa ametawala katika Heshiboni, ambaye Musa alikuwa amemshinda pamoja na viongozi wa Midiani, Evi, Rekemu, Zuri, Huri na Reba, wana wa mfalme wa Sihoni, ambao walikuwa wameishi katika nchi.
22Pia, watu wa Israeli walimwua kwa upanga Baalam mwana wa Beori, ambaye alifanya mambo ya uaguzi, miongoni mwa wale waliowaua.

Read Yoshua 13Yoshua 13
Compare Yoshua 13:10-22Yoshua 13:10-22