Text copied!
CopyCompare
Biblia ya Kiswahili - Wimbo wa Sulemani

Wimbo wa Sulemani 1

Help us?
Click on verse(s) to share them!
1Wimbo ulio Bora, ambao ni wa Sulemani. Wanamke mdogo akizungumza na mpenzi wake
2O, laiti ungenibusu na mabasu ya mdomo wako, kwa kuwa upendo wako ni bora kuliko mvinyo.
3Mafuta yako ya upako yana manukato mazuri; jina lako ni kama marashi yaeleayo, hivyo wanawake wadogo wanakupenda.
4Nichukuwe kwako, na tutakimbia. Mwanamke akizungumza mwenyewe Mfalme amenipeleka vyumbani mwake. Mwanamke akizungumza na mpenzi wake nina furuha; nina furahi kuhusu wewe; acha ni shereheke upendo wako; ni bora kuliko mvinyo. Ni halisi kwa wanawake wengine kupenda. Mwanamke akizungumza na wanawake wengine.
5Mimi ni mweusi lakini mzuri, enyi mabinti wa wanaume wa Yerusalemu - mweusi kama hema za Kedari, muzuri kama mapazia ya Sulemani.
6Usinishangae kwasababu ni mweusi, kwasababu jua limeniunguza. Wana wa mama yangu walikuwa na hasira juu yangu; walinifanya mtunzi wa mashamba ya mizabibu, lakini mshamba langu la mizabibu sijatunza. Wanamke akizungumza na mpenzi wake.
7Niambie, wewe ninaye kupenda, wapi unalisha mifugo yako? Wapi unapumzisha mifugo yako mchana? Kwa nini niwe kama mtu anaye akangaika miongoni mwa mifugo ya marafiki zako? Mpenzi wake anamjibu
8Kama haujui, uliye mzuri miongoni mwa wanawake, fuata nyayo za mifugo yangu, na ulishe watoto wako wa mbuzi karibu na hema za wachungaji.
9Nina kulinganisha, mpenzi wangu, na farasi mzuri wakike miongoni mwa farasi wa magari ya Farao.
10Mashavu yako ni mazuri na mapambo, shingo yako na mikufu ya madini.
11Nitakufanyia mapambo ya dhahabu yaliochanganywa na fedha. Mwanamke akiongea mwenyewe.
12Wakati mfalme akiwa amelala kitandani mwake, marashi yangu yakasambaza arufu.
13Mpenzi wangu ni kwangu kama mkebe wa marashi unao lala usiku katika ya maziwa yangu.
14Mpenzi wangu ni kwangu kama kifurushi cha maua ya hena katika mashamba ya mizabibu ya Eni Gedi. Mpenzi wake anazungumza naye
15Ona, wewe ni mzuri, mpenzi wangu; ona, wewe ni mzuri; macho yako ni kama ya hua. Mwanamke anazungumza na mpenzi wake.
16Ona, wewe ni mtanashati, mpenzi wangu, jinsi mtanashati.
17Nguzo za nyumba yetu ni za matawi ya mierezi, na dari letu ni la matawi ya miberoshi.