Text copied!
CopyCompare
Biblia ya Kiswahili - Waefeso

Waefeso 2

Help us?
Click on verse(s) to share them!
1Kama vile mlivyo kuwa mmekufa katika makosa na dhambi zenu.
2Ilikuwa katika haya kwamba kwanza mlienenda kulingana na nyakati za ulimwengu huu. Mlikuwa mkienenda kwa kufuata mtawala wa mamlaka ya anga. Hii ndiyo roho yake yule afanyaye kazi katika wana wa kuasi.
3Sisi wote hapo mwanzo tulikuwa miongoni mwa hawa wasioamini. Tulikuwa tukitenda kwa namna ya tamaa mbaya za miili yetu. Tulikuwa tukifanya mapenzi ya mwili na ufahamu wetu. Tulikuwa kwa asili wana wa ghadhabu kama wengine.
4Lakini Mungu ni mwingi wa rehema kwa sababu ya pendo lake kubwa alilotupenda sisi.
5Wakati tulipokuwa wafu katika makosa yetu, alituleta pamoja katika maisha mapya ndani ya Kristo. Ni kwa neema kwamba mmeokolewa.
6Mungu alitufufua pamoja na kutufanya kukaa pamoja katika mahali pa mbingu ndani ya Kristo Yesu.
7Alifanya hivi ili katika nyakati zijazo aweze kutuonesha utajiri mkuu wa neema yake. Hutuonesha sisi hili kwa njia ya wema wake ndani ya Kristo Yesu.
8Kwa neema mmeokolewa kwa njia ya imani. Na hii haikutoka kwetu. Ni zawadi ya Mungu.
9Haitokani na matendo. Matokeo yake, asiwepo mmoja wapo wa kujisifu.
10Kwa sababu sisi tu kazi ya Mungu, tumeumbwa katika Kristo Yesu kutenda matendo mema. Ni matendo haya ambayo Mungu aliyapanga tangu zamani za kale kwa ajili yetu, ili tutembee katika hayo.
11Kwa hiyo kumbukeni kwamba hapo zamani mlikuwa watu wa Mataifa kwa jinsi ya mwili. Mnaitwa “msio na tohara” kwa kile kinachoitwa tohara ya mwili inayofanywa kwa mikono ya binadamu.
12Kwa wakati huo mlikuwa mmetengwa na Kristo. Mlikuwa wageni kwa watu wa Israel. Mlikuwa wageni kwa agano la ahadi. Hamkuwa na uhakika wa wakati ujao. Mlikuwa bila Mungu katika ulimwengiu.
13Lakini sasa katika Kristo Yesu ninyi ambao hapo mwanzo mlikuwa mbali na Mungu mmeletwa karibu na Mungu kwa damu ya Kristo.
14Kwa maana yeye ndiye amani yetu. Alifanya wawili kuwa mmoja. Kwa mwili wake aliuharibu ukuta wa utengano ambao ulikuwa umetutenganisha, huo uadui.
15Kwamba alikomesha sheria ya amri na kanuni ili kwamba aumbe mtu mmoja mpya ndani yake. Akafanya amani.
16Alifanya hivi ili kuwapatanisha makundi mawili ya watu kuwa mwili mmoja kwa Mungu kupitia msalaba. Kwa njia ya msalaba aliufisha uadui.
17Yesu alikuja na kutangaza amani kwenu ninyi mliokuwa mbali na amani kwao wale waliokuwa karibu.
18Kwa maana kwa njia ya Yesu sisi wote wawili tuna nafasi kwa yule Roho mmoja kuingia kwa Baba.

19Hivyo basi, ninyi watu wa mataifa si wasafiri na wageni tena. Bali ni wenyeji pamoja na wale waliotengwa kwa ajili ya Mungu na wajumbe katika nyumba ya Mungu.
20Mmejengwa juu ya msingi wa mitume na manabii. Kristo Yesu mwenyewe alikuwa jiwe kuu la pembeni.
21Katika yeye jengo lote limeungamanishwa pamoja na kukua kama hekalu ndani ya Bwana.
22Ni ndani yake ninyi nanyi mnajengwa pamoja kama mahali pa kuishi pa Mungu katika Roho.