Text copied!
CopyCompare
Biblia ya Kiswahili - Waefeso

Waefeso 5

Help us?
Click on verse(s) to share them!
1Kwa hiyo muwe watu wa kumfuata Mungu, kama watoto wake wapendwao.
2Mtembee katika pendo, vilevile kama Kristo alivyotupenda sisi, alijitoa mwenyewe kwa ajili yetu. Yeye alikuwa sadaka na dhabihu, kuwa harufu nzuri ya kumfurahisha Mungu.
3Zinaa au uchafu wowote na tamaa mbaya lazima visitajwe kati yenu, kama inavyotakiwa kwa waaminio,
4wala machukizo yasitajwe, mazungumzo ya kipumbavu, au mizaha ya udhalilishaji, ambayo siyo sawa, badala yake iwepo shukrani.
5Mnaweza kuwa na uhakika ya kwamba kuna zinaa, uchafu, wala atamaniye, huyo nimwabudu sanamu, hana urithi wowote katika ufalme wa Kristo na Mungu.
6Mtu yote asikudanganye kwa maneno matupu, kwa sababu ya mambo haya hasira ya Mungu inakuja juu ya wana wasiotii.
7Hivyo usishiriki pamoja nao.
8Kwa kuwa ninyi mwanzo mlikuwa giza, lakini sasa mmekuwa nuru katika Bwana. Hivyo tembeeni kama watoto wa nuru.
9Kwa kuwa matunda ya nuru yanajumuisha uzuri wote, haki na ukweli.
10Tafuta kile kinacho furahisha kwa Bwana.
11Usiwepo ushiriki katika kazi za giza zisizo na matunda, badala yake ziweke wazi.
12Kwa sababu mambo yanayofanywa na wao sirini ni aibu sana hata kuyaelezea.
13Mambo yote, yanapofichuliwa na nuru, huwa wazi,
14kwa kuwa Kila kitu kilichofichuliwa kinakuwa nuruni. Hivyo husema hivi, “Amka, wewe uliyelala, na inuka kutoka wafu na Kristo atang'aa juu yako.”
15Hivyo iweni makini jinsi mtembeavyo, siyo kama watu wasio werevu bali kama werevu.
16Ukomboeni muda kwa kuwa siku ni za uovu.
17Msiwe wajinga, badala yake, fahamuni nini mapenzi ya Bwana.
18Msilewe kwa mvinyo, huongoza kwenye uharibifu, badala yake mjazwe na Roho Mtakatifu.

19Zungumzeni na kila mmoja wenu kwa zaburi, na sifa, na nyimbo za rohoni. Imbeni na sifuni kwa moyo kwa Bwana.
20Daima toa shukrani kwa mambo yote katika jina la Kristo Yesu Bwana wetu kwa Mungu Baba.
21Jitoeni wenyewe kila mmoja kwa mwingine kwa heshima ya Kristo.
22Wake, jitoeni kwa waume zenu, kama kwa Bwana.
23Kwa sababu mume ni kichwa cha mke, kama Kristo alivyo kichwa cha kanisa. Ni mwokozi wa mwili.
24Lakini kama kanisa lilivyo chini ya Kristo, vilevile wake lazima wafanye hivyo kwa waume zao katika kila jambo.
25Waume, wapendeni wake zenu kama vile Kristo alivyolipenda kanisa na akajitoa mwenyewe kwa ajili yake.
26Alifanya hivyo ili liwe takatifu. Alilitakasa kwa kuliosha na maji katika neno.
27Alifanya hivi ili kwamba aweze kujiwasilishia mwenyewe kanisa tukufu, pasipo na doa wala waa au kitu kifananacho na haya, badala yake ni takatifu lisilo na kosa.
28Kwa njia ile ile, waume wanatakiwa kuwapenda wake zao kama miili yao. Yule ampendae mke wake anajipenda mwenyewe.
29Hakuna hata mmoja anayechukia mwili wake. Badala yake, huurutubisha na kuupenda, kama Kristo pia alivyolipenda kanisa.
30Kwa kuwa sisi ni washiriki wa mwili wake.
31“Kwa sababu hii mwanaume atamwacha baba yake na mama yake na ataungana na mke wake, na hao wawili watakuwa mwili mmoja”.
32huu ulikuwa umefichika. Lakini ninasema kuhusu Kristo na kanisa.
33Walakini, kila mmoja wenu lazima ampende mke wake kama mwenyewe, na mke lazima amheshimu mumewe.