Text copied!
CopyCompare
Biblia ya Kiswahili - Waefeso

Waefeso 6

Help us?
Click on verse(s) to share them!
1Watoto watiini wazazi wenu katika Bwana, kwa maana hii ni haki.
2“Mheshimu baba yako na mama yako” (Maana hii ndiyo amri ya kwanza yenye ahadi),
3“ili iwe heri kwenu na muweze kuishi maisha marefu juu ya nchi.”
4Na ninyi akina baba, msiwakwaze watoto na kuwasababishia hasira, badala yake, waleeni katika maonyo na maagizo ya Bwana.
5Enyi watumwa, iweni watiifu kwa mabwana zenu wa hapa duniani kwa heshima kubwa na kutetemeka kwa hofu itokayo mioyoni mwenu. muwe watiifu kwao kama vile mnavyomtii Kristo.
6Utii wenu usiwe tu pale mabwana zenu wanapowatazama ili kuwafurahisha. Badala yake, iweni watiifu kama watumwa wa Kristo. Fanyeni Mapenzi ya Mungu kutoka mioyoni mwenu,
7watumikieni kwa mioyo yenu yote, kwa kuwa mnamtumikia Bwana na wala si wanadamu,
8mnapaswa kujua kwamba katika kila tendo jema mtu analofanya, atapokea zawadi kutoka kwa Bwana, ikiwa ni mtumwa au mtu huru.
9Na ninyi mabwana fanyeni vivyo hivyo kwa watumwa wenu. Msiwatishe mkijua kwamba yeye aliye Bwana wa wote ni yule aliye mbinguni. Mkijua kuwa hakuna upendeleo ndani yake.
10Hatimaye, iweni na nguvu katika Bwana na katika uwezo wa nguvu zake.
11Vaeni silaha zote za Mungu, ili kwamba mpate kusimama kinyume na hila za shetani.
12kwa kuwa vita yetu si ya damu na nyama, bali ni dhidi ya falme na mamlaka ya roho na watawala wa ulimwengu wa uovu na giza, dhidi ya pepo katika sehemu za mbingu.
13Kwa hiyo, vaeni silaha zote za Mungu, ili mpate kusimama imara dhidi ya uovu katika kipindi hiki kiovu. Baada ya kumaliza kila kitu, mtasimama imara.
14Hatimaye simameni imara. Fanyeni hivi baada ya kuwa mmefunga mkanda katika kweli na haki kifuani.
15Fanyini hivi mkiwa mmevaa utayari miguuni mwenu wa kutangaza injili ya amani.
16Katika kila hali mkichukua ngao ya imani, ambayo itakuwezesha kuizima mishale ya yule mwovu.
17Vaeni kofia ya wokovu na upanga wa Roho, ambayo ni neno la Mungu.
18pamoja na maombi na dua. Ombeni kwa Roho kila wakati. Kwa mtazamo huu iweni waangalifu kila wakati kwa uvumilivu wote na maombi kwa ajili ya waamini wote.

19Ombeni kwa ajili yangu, ili nipewe ujumbe ninapofungua mdomo wangu. Ombeni kwamba nieleweshe kwa ujasiri kweli iliyofichika ihusuyo injili.
20Ni kwa ajili ya injili mimi ni balozi niliyefungwa minyororo, ili kwamba ndani mwao niseme kwa ujasiri kama ninavyowiwa kusema.
21Lakini ninyi pia mjue mambo yangu na jinsi ninavyoendelea, Tikiko ndugu yangu kipenzi na mtumishi mwaminifu katika Bwana, atawajulisha kila kitu.
22Nimemtuma kwenu kwa kusudi hili maalumu, ili kwamba mjue mambo kuhusu sisi, aweze kuwafariji mioyo yenu.
23Amani na iwe kwa ndugu, na upendo pamoja na imani kutoka kwa Mungu baba na Bwana Yesu Kristo.
24Neema na iwe pamoja na wote wanampenda Bwana Yesu Kristo kwa pendo lile lisilo kufa.