Text copied!
CopyCompare
Biblia ya Kiswahili - Luka - Luka 9

Luka 9:16-37

Help us?
Click on verse(s) to share them!
16Akachukua mikate mitano na samaki wawili na akatazama mbinguni, akavibariki, na kuvimega katika vipande, akawapa wanafunzi wake ili waviweke mbele ya makutano.
17Wote wakala na wakashiba, na vipande vya chakula vilivyo baki viliokotwa na kujaza vikapu kumi na viwili.
18Nayo ikawa kwamba, alipokuwa akiomba peke yake, wanafunzi wake walikuwa pamoja naye, na akawauliza akisema, “watu husema mimi ni nani?”
19Wakijibu, wakasema, “Yohana mbatizaji, lakini wengine husema Eliya, na wengine husema mmoja wa manabii wa nyakati za zamani amefufuka tena.”
20Akawambia, “Lakini ninyi mwasema mimi ni nani?” Akijibu Petro akasema, “Kristo kutoka kwa Mungu.”
21Lakini kwa kuwaonya, Yesu akawaelekeza kutomwambia yeyote juu ya hili,
22akasema kwamba mwana wa Adamu lazma ateseke kwa mambo mengi na kukataliwa na wazee na Makuhani wakuu na waandishi, na atauawa, na siku ya tatu atafufuka.
23Akawambia wote, “kama mtu yeyote akitaka kunifuata, lazima ajikane mwenyewe, achukue msalaba wake kila siku, na anifuate.
24Yeyote ajaribuye kuyaokoa maisha yake atayapoteza, lakini yeyote apotezae maisha yake kwa faida yangu, atayaokoa.
25Je kitamfaidia nini mwanadamu, kama akiupata ulimwengu wote, lakini akapoteza au akapata hasara ya nafsi yake?
26Yeyote atakaye nionea aibu mimi na maneno yangu, kwake yeye mwana wa Adam atamuonea aibu atakapo kuwa katika utukufu wake, na utukufu wa Baba na malaika watakatifu.
27Lakini ninawaambia ukweli, kuna baadhi yenu wasimamao hapa, hawata onja umauti mpaka wauone ufalme wa Mungu.”
28Ikatokea yapata siku nane baada ya Yesu kusema maneno haya kwamba akawachukua pamoja nae Petro, Yohana na, Yakobo, wakapanda mlimani kuomba.
29Na alipokuwa katika kuomba, muonekano wa uso wake ulibadilika, na mavazi yake yakawa meupe na ya kung'aa.
30Na tazama, walikuwepo wanaume wawili wakiongea naye! Walikuwa Musa na Elia,
31walionekana katika utukufu. Waliongea kuhusu kuondoka kwake, jambo ambalo alikaribia kulitimiza Yerusalem.
32Sasa Petro na wale waliokua pamoja naye walikuwa katika usingizi mzito. Lakini walipokuamka, waliuona utukufu wake na wanaume wawili waliokuwa wamesimama pamoja nae.
33Ikatokea kwamba, walipokuwa wakiondoka kwa Yesu, Petro akamwambia, “Bwana, ni vizuri kwetu kukaa hapa na inatupasa tutengeneze makazi ya watu watatu. Tutengeneze moja kwa ajili yako, moja kwa ajili ya Musa, na moja kwa ajili ya Eliya.” Hakuelewa alichokuwa akiongelea.
34Alipokuwa akisema hayo, likaja wingu na likawafunika; na waliogopa walipoona wamezunguwa na wamezungukwa na wingu.
35Sauti ikatoka kwenye wingu ikasema, “Huyu ni Mwanangu mteule. Msikilizeni yeye.”
36Sauti iliponyamaza, Yesu alikuwa peke yake. walikaa kimya, na katika siku hizo hawakumwambia yeyote lolote miongoni mwa waliyoyaona.
37Siku iliyofuata, baada ya kutoka mlimani, kusanyiko kubwa la watu lilikutana naye.

Read Luka 9Luka 9
Compare Luka 9:16-37Luka 9:16-37