19Kama utakubali na kutii, utakula mema ya nchi,
20lakini ukikataa na kugeuka, upanga utakuangamiza, maama Yahwe amesema.
21Ni kwa jinsi gani mji ulioaminika umekuwa kahaba! ulikuwa ni mij wenye usawa na haki, lakini sasa mji umejaa mauwaji.
22Fedha zenu zimechafuka, na mvinyo wenu umechanganjwa na maji.
23Viongozi wenu wamemgeuka Mungu wamekuwa marafiki wa wezi; yeyote anayopenda rushwa na kuikimbilia. Hawawajali yatima, wala wajane wanaokuja kuwanyenyekea mbele yao.