6Mbwa mwitu atakaa pamoja na kondoo, na chui watalala chini pamoja na mtoto wa mbuzi, ndama, mtoto wa simba na ndama pamoja na ndama aliyenona. Mtoto mdogo atawaongoza wao.
7Ng'ombe na dubu watachungwa pamoja. Na watoto wao watalala pamoja. Simba atakula majani kama ng'ombe.
8Mtoto atacheza juu ya chimo la nyoka, na mtoto aliyeachwa ataweka mkono wake katika pango la nyoka.
9Hawataumizwa wala kuharibiwa kwenye mlima mtakatifu; kwa maana dunia itakuwa imejaa maarifa ya Yahwe, kama maji yajaavyo kwenye bahari.
10Siku hiyo mzizi wa Yese utasimama kama bendera ya watu. Taifa litamtafuta yeye nje, na mahali pake pakupumzikia patatukuka.
11Siku hiyo, Bwana ataunyoosha mkono wake tena kuokoa mabaki ya watu wake yaliyosalia huko Asiria, Misri, Pathrosi, Kushi, Shinari, Hamathi, na kisiwa cha bahari.
12Ataweka bendera kwa kwa mataifa na atakusanya Waisrel waliotupwa na watu wa Juuda waliotawanyika kitika pembe nne za dunia.