13Kwa maana amesema, ''Kwa nguvu zangu na kwa hekima yangu niliyoifanya. na Nimeelewa, na nimeondoa mipaka ya watu. nimewaibia akiba yao, ni kama nilioileta chini kwa wenyeji wake.
14Na mkono wangu umezitoa mali za mataifa kama vile mtu ayakusanyavyo mayai, kama nilivyokusanya dunia yote. Hakuna atakayeperusha mabawa yake au kufungua midomo yake au kulia.''
15Je shoka lijisifu lenyewe juu ya mtu anayelitumia? Je litajisifia lenyewe zaidi ya yule anaelitumia kukatia? Au fimbo imuinuae yeye ambaye si mti.