Text copied!
CopyCompare
Biblia ya Kiswahili - Yoshua - Yoshua 10

Yoshua 10:22-36

Help us?
Click on verse(s) to share them!
22Kisha Yoshua akasema, “Fungueni mlango wa pango, watoeni nje na waleteni kwangu hawa wafalme watano.”
23Walifanya kama Yoshua alivyosema. Waliwaleta wafalme watano kutoka katika pango - mfalme wa Yerusalemu, mfalme wa Hebroni, mfalme wa Yarmuthi, mfalme wa Lakishi na mfalme wa Egloni.
24Na walipowaleta wafalme kwa Yoshua, alimwita kila mtu wa Israeli, na aliwaambia maakida wa wanajeshi waliokuwa wameenda vitani pamoja naye “Kanyageni miguu yenu juu ya shingo zao.” Basi walikuja na kukanyaga miguu yao juu ya shingo zao.
25Kisha akawaambia, 'Msiogope wala kufadhaika. uwe na moyo mkuu na jasiri. Na hiki ndicho Mungu atakachokifanya kwa maadui wenu wote ambao mtapigana nao'.
26Kisha Yoshua akawashambulia na kuwaua wafalme. Aliwatundika wote watano juu ya miti. Waliwatundika juu ya miti hata jioni.
27Ilipokuwa jioni, Yoshua alitoa maagizo, nao waliwashusha chini ya miti na kisha wakawatupa katika pango ambalo walikuwa wamejificha wao wenyewe. Waliweka mawe makubwa juu ya mlango wa pango. Mawe hayo yapo pale hadi leo hii.
28Na kwa namna hii, katika siku hiyo Yoshua aliuteka mji wa Makeda na aliwaua watu wote huko kwa upanga, pamoja na mfalme wake. Aliwateketeza wote kabisa pamoja na kila kiumbe hai kilichokuwa huko. Hakuna hata mmoja aliyesalia. Alichomfanyia mfalme wa Makeda ni sawa sawa na kile alichokuwa amemfanyia mfalme wa Yeriko.
29Yoshua na Israeli wote waliipita Makeda na kufika Libna. Na huko waliingia katika vita dhidi ya Libna.
30Yahweh pia aliitia katika mkono wa Israeli pamoja na mfalme wake. Yoshua alishambulia kila kiumbe hai ndani yake kwa upanga. Hakuacha hai hata mtu mmoja. Alichomfanyia mfalme ni sawa sawa na kile alichokuwa amemfanyia mfalme wa Yeriko.
31Baadaye Yoshua na Israeli wote pamoja naye walipanda kutoka Libna na kwenda Lakishi. Alipiga kambi karibu yake na wakafanya vita dhidi yake.
32Yahweh aliitia Lakishi katika mkono wa Israeli. Yoshua aliiteka katika siku ya pili. Alishambulia kwa upanga kilia kiumbe hai kilichokuwa ndani yake, kama vile aliyokuwa amefanya huko Libna.
33Kisha Horamu, mfalme wa Gezeri alikwea ili kuisaida Lakishi. Yoshua alimshambulia yeye na jeshi lake mpaka pale ambapo hapakuwa na mtu hata mmoja aliyesalia.
34Baada ya hapo, Yoshua na Israeli wote walitoka Lakishi na kwenda Egloni. Walipiga kambi karibu yake na kisha wakafanya vita dhidi yake,
35na siku hiyo hiyo wakaiteka. Waliupiga kwa upanga na waliteketeza kila mtu ndani yake kama vile Yoshua alivyofanya huko Lakishi.
36Kisha Joshua na Israeli wote wakatoka Egloni na kwenda Hebroni. Wakainua vita dhidi yake.

Read Yoshua 10Yoshua 10
Compare Yoshua 10:22-36Yoshua 10:22-36