8Majirani wa yule mtu na wale waliomuona mwanzo kama mwombaji walisema, Je! huyu siye yule mtu aliyekuwa akikaa na kuomba?” wengine walisema, “Ni yeye.”
9Na wengine walisema, “Hapana, bali anafanana naye.” Lakini alikuwa akisema, “Ni mimi.”
10Wakamwambia, “Sasa macho yako yalifunguliwaje?”
11Alijibu, mtu aitwaye Yesu alifanya tope na kupaka macho yangu na kuniambia, 'Nenda Siloam ukanawe.' Kwa hiyo nilienda, na nikanawa, na nikapata kuona tena.”
12Wakamwambia, “Yuko wapi?” Alijibu, “Sijui.”
13Wakampeleka yule mtu aliyewahi kuwa kipofu kwa Mafarisayo.