Text copied!
CopyCompare
Biblia ya Kiswahili - Warumi - Warumi 3

Warumi 3:5-27

Help us?
Click on verse(s) to share them!
5Lakini ikiwa uovu wetu unaonesha haki ya Mungu, tuseme nini? Mungu si dhalimu atoapo ghadhabu yake, je yupo hivyo? Naongea kutokana na mantiki ya kibinadamu.
6La hasha! Ni jinsi gani basi Mungu atauhukumu ulimwengu?
7Lakini ikiwa kweli ya Mungu kupitia uongo wangu hutoa sifa tele kwa ajili yake, kwa nini ningali bado nahukumiwa kama mwenye dhambi?
8Kwa nini tusiseme, kama tulivyosingiziwa na kama wengine wanavyothibitisha kwamba tunasema, “Tufanye uovu, ili mema yaje”? Hukumu juu yao ni ya haki.
9Ni nini basi? Tunajitetea wenyewe? Hapana kabisa. Kwa kuwa sisi tayari tumewatuhumu Wayahudi na Wayunani wote pamoja, ya kuwa wapo chini ya dhambi.
10Hii ni kama ilivyoandikwa: “Hakuna mwenye haki, hata mmoja.
11Hakuna mtu ambaye anaelewa. Hakuna mtu ambaye anamtafuta Mungu.
12Wote wamegeuka. Wao kwa pamoja wamekuwa hawana maana. Hakuna atendaye mema, la, hata mmoja.
13Makoo yao ni kaburi lililo wazi. Ndimi zao zimedanganya. Sumu ya nyoka ipo chini ya midomo yao.
14Vinywa vyao vimejaa laana na uchungu.
15Miguu yao ina mbio kumwaga damu.
16Uharibifu na mateso yapo katika njia zao.
17Watu hawa hawajajua njia ya amani.
18Hakuna hofu ya Mungu mbele ya macho yao.”
19Sasa tunajua kwamba chochote sheria isemacho, husema na wale walio chini ya sheria. Hii ni ili kwamba kila kinywa kifungwe, na hivyo kwamba ulimwengu wote uweze kuwajibika kwa Mungu.
20Hii ni kwa sababu hakuna mwili utakaohesabiwa haki kwa matendo ya sheria mbele za macho yake. Kwa kuwa kupitia Sheria huja ufahamu wa dhambi.
21Lakini sasa pasipo sheria, haki ya Mungu imejulikana. Ilishuhudiwa kwa sheria na Manabii,
22hiyo ni, haki ya Mungu kupitia imani katika Yesu Kristo kwa wale wote wanaoamini. Maana hakuna tofauti.
23Kwa kuwa wote wamefanya dhambi, na kupungukiwa na utukufu wa Mungu.
24Wamehesabiwa haki bure kwa neema yake kwa njia ya ukombozi ulio katika Kristo Yesu.
25Kwa maana Mungu alimtoa Kristo Yesu awe upatanisho kwa njia ya imani katika damu yake. Alimtoa Kristo kama ushahidi wa haki yake, kwa sababu ya kuziachilia dhambi zilizopita
26katika uvumilivu wake. Haya yote yalitokea ili kuonesha haki yake wakati huu wa sasa. Hii ilikuwa ili aweze kujithibitisha mwenyewe kuwa haki, na kuonesha kwamba humhesabia haki mtu yeyote kwa sababu ya imani katika Yesu.
27Kuwapi basi kujisifu? Kumetengwa. Kwa misingi ipi? Misingi ya matendo? Hapana, lakini kwa misingi ya imani.

Read Warumi 3Warumi 3
Compare Warumi 3:5-27Warumi 3:5-27