Text copied!
CopyCompare
Biblia ya Kiswahili - Warumi

Warumi 13

Help us?
Click on verse(s) to share them!
1Kila nafsi na iwe na utii kwa mamlaka ya juu, kwa kuwa hakuna mamlaka isipokuwa imetoka kwa Mungu. Na mamlaka zilizopo zimewekwa na Mungu.
2Kwa hiyo ambaye anapinga mamlaka hiyo hupinga amri ya Mungu; na wale waipingao watapokea hukumu juu yao wenyewe.
3Kwa kuwa watawala si tishio kwa watendao mema, bali kwa watendao maovu. Je unatamani kutoogopa mamlaka? Fanya yaliyo mema, na utasifiwa nayo.
4Kwa kuwa ni mtumishi wa Mungu kwako kwa ajili ya mema. Bali kama utatenda yaliyo maovu, ogopa; kwa kuwa habebi upanga bila sababu. Kwa kuwa ni mtumishi wa Mungu, mlipa kisasi kwa ghadhabu juu ya yule afanyaye uovu.
5Kwa hiyo inakupasa utii, si tu kwa sababu ya gadhabu, bali pia kwa sababu ya dhamiri.
6Kwa ajili hii pia unalipa kodi. Kwa kuwa wenye mamlaka ni watumishi wa Mungu, ambao wanaendelea kufanya jambo hili.
7Mlipeni kila mmoja ambacho wanawadai: kodi kwa astahiliye kodi; ushuru kwa astahiliye ushuru; hofu kwa astahiliye hofu; heshima kwa astahiliye heshima.
8Msidaiwe na mtu kitu chochote, isipokuwa kupendana ninyi kwa ninyi. Kwa kuwa yeye ampendaye jirani yake ametimiliza sheria.
9Kwa kuwa, “Hautazini, hautaua, hautaiba, hautatamani,” na kama kuna amri nyingine pia, imejumlishwa katika sentensi hii: “Utampenda jirani yako kama wewe mwenyewe.”
10Upendo hamdhuru jirani wa mtu. Kwa hiyo, upendo ni ukamilifu wa sheria.
11Kwa sababu ya hili, mnajua wakati, kwamba tayari ni wakati wa kutoka katika usingizi. Kwa kuwa wokovu wetu umekaribia zaidi ya wakati ule tulio amini kwanza.
12Usiku umeendelea, na mchana umekaribia. Na tuweke pembeni matendo ya giza, na tuvae silaha za nuru.
13Na tuenende sawa sawa, kama katika nuru, si kwa sherehe za uovu au ulevi. Na tusienende katika zinaa au tamaa isiyoweza kudhibitiwa, na si katika fitina au wivu.
14Bali tumvae Bwana Yesu Kristo, na tusiweke nafasi kwa ajili ya mwili, kwa tamaa zake.