Text copied!
CopyCompare
Biblia ya Kiswahili - Warumi

Warumi 15

Help us?
Click on verse(s) to share them!
1Sasa sisi tulio na nguvu tunapaswa kuuchukua udhaifu wa walio dhaifu, na hatupaswi kujipendeza wenyewe.
2Kila mmoja wetu ampendeze jirani yake kwani ni jambo jema, kwa lengo la kumjenga.
3Kwani hata Kristo hakujipendeza mwenyewe. Badala yake, ilikuwa kama ilivyoandikwa, “Matusi ya wale waliokutukana yamenipata mimi.”
4Kwa chochote kilichotangulia kuandikwa, kiliandikwa kwa kutuelekeza, kwa kusudi kwamba kupitia uvumilivu na kupitia kutiwa moyo na maandiko tungekuwa na ujasiri.
5Sasa Mungu wa uvumilivu na wa kutia moyo awape kuwa na nia sawa kwa kila mmoja kulingana na Yesu Kristo.
6Aweze kufanya hivi kwa nia moja muweze kumsifu kwa kinywa kimoja Mungu na Baba wa Bwana wetu Yesu Kristo.
7Kwa hiyo mpokeeni kila mmoja, kama vile Kristo alivyowapokea, kwa utukufu wa Mungu.
8Kwani nasema kwamba Kristo amefanywa mtumishi wa tohara kwa niaba ya ukweli wa Mungu. Alifanya hivi ili kwamba aweze kuthibitisha ahadi zilizotolewa kwa mababa,
9na kwa mataifa kumtukuza Mungu kwa neema yake. Kama ambavyo imeandikwa, “Kwa hiyo nitatoa sifa kwako miongoni mwa mataifa na kuimba sifa katika jina lako.”
10Tena inasema, “Furahini, ninyi watu wa mataifa, pamoja na watu wake.”
11Na tena, “Msifuni Bwana, ninyi mataifa yote; acha watu wa mataifa yote wamsifu yeye.”
12Tena Isaya asema, “Kutakuwa na shina la Yese, na mmoja atakayeinuka kutawala juu ya mataifa. Mataifa watakuwa na tumaini katika yeye.”
13Sasa Mungu wa tumaini awajaze na furaha yote na amani kwa kuamini, ili kwamba muweze kuzidi katika tumaini, kwa nguvu ya Roho Mtakatifu.
14Mimi mwenyewe pia nimeshawishiwa nanyi, ndugu zangu. Nimeshawishiwa kwamba pia ninyi wenyewe mmejazwa na wema, mmejazwa na maarifa yote. Ninashawishiwa kwamba, ninyi mwaweza pia kuhimizana kila mmoja na mwenzake.
15Lakini ninaandika kwa ujasiri zaidi kwenu juu ya mambo fulani ili kuwakumbusha tena, sababu ya kipawa nilichopewa na Mungu.
16Kipawa hiki kilikuwa kwamba niweze kuwa mtumishi wa Yesu Kristo aliyetumwa kwa mataifa, kujitoa kama kuhani wa injili ya Mungu. Ningeweza kufanya hivi ili kujitoa kwangu kwa mataifa kuwe kumekubaliwa, kumetengwa na Mungu kwa njia ya Roho Mtakatifu.
17Hivyo furaha yangu iko katika Kristo Yesu na katika mambo ya Mungu.
18Kwani sitaweza kuthubutu kunena lolote isipokuwa kwamba Kristo amekamilisha kupitia kwangu utii wa mataifa. Haya mambo yametimizwa kwa neno na tendo,

19kwa nguvu za ishara na maajabu, na kwa nguvu za Roho Mtakatifu. Hii ilikuwa ili kwamba kutoka Yerusalem, na kuzungukia mbali kama Iliriko, niweze kuichukua nje kwa ukamilifu injili ya Kristo.
20Kwa njia hii, nia yangu imekuwa kuitangaza injili, lakini si mahali Kristo anajulikana kwa jina, ili kwamba nisiweze kujenga juu ya msingi wa mtu mwingine.
21Kama ilivyoandikwa: “Ambao kwa yeye hawana habari zake alikuja watamwona, na wale ambao hawakumsikia watamfahamu.”
22Kwahiyo nilikuwa pia nimezuiliwa mara nyingi kuja kwenu.
23Lakini sasa, sina tena sehemu yoyote katika mikoa hii, na nimekuwa nikitamani kwa miaka mingi kuja kwenu.
24Hivyo mara zote nikienda Hispania, ninatumaini kuwaona nikipita, na kuweza kupelekwa njia yangu na ninyi, baada ya kuwa nimefurahia ushirika na ninyi kwa muda.
25Lakini sasa ninakwenda Yerusalemu kuwahudumia waumini.
26Maana iliwapendeza watu wa Makedonia na Akaya kufanya changizo maalumu kwa masikini miongoni mwa waumini huko Yerusalemu.
27Ndiyo, ilikuwa kwa upendo wao, na hakika, wamekuwa wadeni wao. Maana ikiwa mataifa wameshiriki katika mambo yao ya kiroho, wanadaiwa na wao pia kuwahudumia katika mahitaji ya vitu.
28Kwahiyo, wakati nimekamilisha hivi na kuwa na utoshelevu wa tunda hili kwao, mimi nitakwenda njiani pamoja nanyi huko Hispania.
29Najua kwamba, wakati nikija kwenu, nitakuja katika utimilifu wa baraka za Kristo.
30Sasa ninawasihi, ndugu, kwa Bwana wetu Yesu Kristo, na kwa upendo wa Roho, kwamba mshiriki pamoja nami katika maombi yenu kwa Mungu kwa ajili yangu.
31Ombeni kwamba niweze kuokolewa kutoka kwao wasio na utii katika Yudea, na kwamba huduma yangu huko Yerusalemu iweze kupokelewa na waumini.
32Ombeni kwamba ninaweza kuja kwenu kwa furaha kupitia mapenzi ya Mungu, na kwamba niweze kuwa pamoja nanyi, kupata kupumzika.
33Na Mungu wa amani awe pamoja nanyi nyote. Amina