Text copied!
CopyCompare
Biblia ya Kiswahili - Matendo ya Mitume - Matendo ya Mitume 27

Matendo ya Mitume 27:1-25

Help us?
Click on verse(s) to share them!
1Ilipoamuliwa kwamba tunatakiwa tusafiri kwa maji kwenda Italia, walimkabidhi Paulo na wafungwa wengine kwa afisa mmoja wa jeshi la Kiroma aliyeitwa Julio, wa Kikosi cha Agustani.
2Tukapanda meli kutoka Adramitamu, ambayo ilikuwa isafiri kandokando ya pwani ya Asia. Hivyo tukaingia baharini. Aristaka kutoka Thesolanike ya Makedonia akaenda pamoja nasi.
3Siku iliyofuata tukatua nanga katika mji wa Sidoni, ambapo Julio alimtendea Paulo kwa ukarimu na akamruhusu kwenda kwa rafiki zake kupokea ukarimu wao.
4Kutoka hapo tukaenda baharini tukasafiri kuzunguka kisiwa cha Kipro ambacho kilikuwa kimeukinga upepo, kwa sababu upepo ulikuwa ukitukabili.
5Baada ya kuwa tumesafiri katika maji yaliyo karibu na Kilikia na Pamfilia, tukaja Mira, mji wa Lisia.
6Pale yule afisa wa jeshi la Kiroma, akaikuta meli kutoka Alexandria ambayo ilikuwa isafiri kuelekea Italia. Akatupandisha ndani yake.
7Baada ya kuwa tumesafiri polepole kwa siku nyingi na hatimaye tukawa tumefika kwa taabu karibu na Kinidas, upepo haukuturuhusu tena kuelekea njia hiyo, hivyo tukasafiri kandokando ya kivuli cha Krete tukiukinga upepo, mkabala na Salmone.
8Tukasafiri kandokando ya pwani kwa ugumu, mpaka tukafika mahali palipoitwa Fari Haveni ambayo iko karibu na mji wa Lasi.
9Tulikuwa tumechukua muda mwingi sana, na muda wa mfungo wa Kiyahudi ulikuwa umepita pia, na sasa ilikuwa ni hatari kuendelea kusafiri. Hivyo Paulo akatuonya,
10na kusema, “Wanaume, naona safari ambayo tunataka tuichukue itakuwa na madhara na hasara nyingi, siyo tu ya mizigo na meli, lakini pia ya maisha yetu.”
11Lakini afisa wa jeshi la Kiroma akamsikiliza zaidi bwana wake na mmiliki wa meli, kuliko mambo yale ambayo yalizungumzwa na Paulo.
12Kwa sababu bandari haikuwa sehemu rahisi kukaa wakati wa baridi, mabaharia wengi wakashauri tusafiri kutoka pale, ili kwa namna yoyote tukiweza kuufikia mji wa Foinike, tukae pale wakati wa baridi. Foinike ni bandari huko Krete, na inatazama kaskazini mashariki na kusini mashariki.
13Upepo wa kusini ulipoanza kuvuma polepole, mabaharia wakafikiri wamepata kile ambacho walikuwa wanakihitaji. Wakang'oa nanga na kusafiri kandokando ya Krete karibu na pwani.
14Lakini baada ya muda mfupi upepo mkali, ulioitwa Wa kaskazini mashariki, ukaanza kutupiga kutoka ng'ambo ya kisiwa.
15Wakati meli ilipolemewa na kushindwa kuukabili upepo, tukakubaliana na hali hiyo, tukasafirishwa nao.
16Tukakimbia kupitia ule upande uliokuwa unaukinga upepo wa kisiwa kiitwacho Kauda; na kwa taabu sana tulifanikiwa kuuokoa mtumbwi.
17Baada ya kuwa wameivuta, walitumia kamba kuifunga meli. Waliogopa kwamba tungeweza kwenda kwenye eneo la mchanga mwingi la Syiti, hivyo wakashusha nanga na waliendeshwa kandokando.
18Tulipigwa kwa nguvu sana na dhoruba, hivyo siku iliyofuata mabaharia wakaanza kutupa mizigo kutoka melini.
19Siku ya tatu, mabaharia wakaanza kuyatoa maji kwa mikono yao wenyewe.
20Wakati ambapo jua na nyota hazikutuangazia kwa siku nyingi, bado dhoruba kubwa ilitupiga, na matumaini kwamba tungeokolewa yalitoweka.
21Baada ya kuwa wameenda muda mrefu bila chakula, hapo Paulo akasimama katikati ya mabaharia akasema, “Wanaume, mlipaswa mnisikilize, na tusingengo'a nanga kutoka Krete, ili kupata haya madhara na hasara.
22Na sasa nawafariji mjitie moyo, kwa sababu hakutakuwa upotevu maisha kati yenu, isipokuwa hasara ya meli tu.
23Kwa sababu usiku uliopita malaika wa Mungu, ambaye huyo Mungu mimi ni wake, na ambaye ninamwabudu pia - malaika wake alisimama pembeni mwangu
24na kusema, “Usiogope Paulo. Lazima usimame mbele ya Kaisari, na tazama, Mungu katika wema wake amekupa hawa wote ambao wanasafiri pamoja nawe.
25Hivyo, wanaume, jipeni moyo, kwa sababu namwamini Mungu, kwamba itakuwa kama nilivyoambiwa.

Read Matendo ya Mitume 27Matendo ya Mitume 27
Compare Matendo ya Mitume 27:1-25Matendo ya Mitume 27:1-25