Text copied!
CopyCompare
Biblia Takatifu - Yohana - Yohana 17

Yohana 17:9-12

Help us?
Click on verse(s) to share them!
9“Nawaombea hao; siuombei ulimwengu, ila nawaombea hao ulionipa, maana ni wako.
10Yote niliyo nayo ni yako, na yako ni yangu; na utukufu wangu umeonekana ndani yao.
11Na sasa naja kwako; simo tena ulimwenguni, lakini wao wamo ulimwenguni. Baba Mtakatifu! Kwa nguvu ya jina lako ulilonipa, tafadhali uwaweke salama ili wawe kitu kimoja kama sisi tulivyo mmoja.
12Nilipokuwa nao, mimi niliwaweka salama kwa nguvu ya jina lako ulilonipa. Mimi nimewalinda, wala hakuna hata mmoja wao aliyepotea, isipokuwa yule aliyelazimika kupotea ili Maandiko Matakatifu yapate kutimia.

Read Yohana 17Yohana 17
Compare Yohana 17:9-12Yohana 17:9-12