Text copied!
CopyCompare
Biblia ya Kiswahili - Warumi - Warumi 16

Warumi 16:1-17

Help us?
Click on verse(s) to share them!
1Namkabidhi kwenu Fibi dada yetu, ambaye ni mtumishi wa kanisa ambalo liko Kenkrea,
2ili kwamba mnaweza kumpokea katika Bwana. Fanyeni hivi katika kicho cha thamani cha waumini, na msimame pamoja naye katika jambo lolote atakalokuwa na uhitaji nalo. Maana yeye mwenyewe amekuwa mhudumu wa wengi, na kwa ajili yangu mwenyewe.
3Msalimu Priska na Akila, watenda kazi pamoja nami katika Kristo Yesu,
4ambao kwa maisha yangu waliyahatarisha maisha yao wenyewe. Ninatoa shukrani kwao, na siyo tu mimi, bali pia kwa makanisa yote ya mataifa.
5Lisalimie kanisa ambalo liko nyumbani kwao. Msalimie Epanieto mpendwa wangu, ambaye ni mzaliwa wa kwanza wa Kristo katika Asia.
6Msalimie Mariamu ambaye ametenda kazi kwa bidii kwa ajili yenu.
7Msalimie Androniko na Yunia, jamaa zangu, na wafungwa pamoja nami. Ni wa muhimu miongoni mwa mitume, ambao pia walitangulia kumjua Kristo kabla yangu.
8Msalimie Ampliato, mpendwa wangu katika Bwana.
9Msalimie Urbano, mtenda kazi pamoja nami katika Kristo, na Stakisi mpendwa wangu.
10Msalimie Apele, mwenye kukubaliwa katika Kristo. Wasalimie wote ambao walio katika nyumba ya Aristobulo.
11Nisalimie Herodioni, jamaa yangu. Nisalimie wote walio katika nyumba ya Narkiso, ambao wako katika Bwana.
12Nisalimie Trifaina na Trifosa, wanaotenda kazi kwa bidii katika Bwana. msalimie Persisi mpendwa, ambaye ametenda kazi zaidi kwa Bwana,
13Nisalimie Rufo, aliyechaguliwa katika Bwana na mama yake na wangu.
14Msalimie Asinkrito, Flegon, Herme, Patroba, Herma, na ndugu wote walio pamoja nao.
15Nisalimie Filologo naYulia, Nerea na dada yake, na Olimpa, na waumini wote walio pamoja nao.
16Nisalimie kila mmoja kwa busu takatifu. Makanisa yote katika Kristo yawasalimu.
17Sasa nawasihi, ndugu, kutafakari juu ya hao ambao wanasababisha mgawanyiko na vipingamizi. Wanakwenda kinyume na mafundisho ambayo mmekwisha kujifunza. Geukeni mtoke kwao.

Read Warumi 16Warumi 16
Compare Warumi 16:1-17Warumi 16:1-17