Text copied!
Bibles in Swahili (individual language)

Warumi 16:1-17 in Swahili (individual language)

Help us?

Warumi 16:1-17 in Biblia Takatifu

1 Napenda kumjulisha kwenu dada yetu Foibe ambaye ni mtumishi katika kanisa la Kenkrea.
2 Mpokeeni kwa ajili ya Bwana kama iwapasavyo watu wa Mungu. Mpeni msaada wowote atakaohitaji kutoka kwenu, maana yeye amekuwa mwema sana kwa watu wengi na kwangu pia.
3 Salamu zangu ziwafikie Priska na Akula, wafanyakazi wenzangu katika utumishi wa Kristo Yesu.
4 Wao walihatarisha maisha yao kwa ajili yangu. Wanastahili shukrani; si tu kutoka kwangu, bali pia kutoka kwa makanisa yote ya watu wa mataifa mengine.
5 Salamu zangu pia kwa kanisa linalokutana nyumbani kwao. Salamu zangu zimfikie rafiki yangu Epaineto ambaye ni kwa kwanza katika mkoa wa Asia kumwamini Kristo.
6 Nisalimieni Maria ambaye amefanya kazi kwa bidii kwa ajili yenu.
7 Salamu zangu kwa Androniko na Yunia, wananchi wenzangu waliofungwa gerezani pamoja nami; wao wanajulikana sana kati ya mitume; tena walikuwa Wakristo kabla yangu mimi.
8 Salamu zangu kwa Ampliato, rafiki yangu katika kuungana na Bwana.
9 Salamu zangu zimfikie Urbano, mfanyakazi mwenzangu katika utumishi wa Kristo; salamu zangu pia kwa rafiki yangu Staku.
10 Nisalimieni Apele ambaye uaminifu wake kwa Kristo umethibitishwa. Salamu zangu kwa wote walio nyumbani mwa Aristobulo.
11 Salamu zangu kwa Herodiana, mwananchi mwenzangu; na kwa jamaa yote ya Narkisi iliyojiunga na Bwana.
12 Nisalimieni Trufena na Trufosa wanaofanya kazi katika utumishi wa Bwana, na rafiki yangu Persi ambaye amefanya mengi kwa ajili ya Bwana.
13 Nisalimieni Rufo, mtu hodari sana katika kazi ya Bwana, na mama yake ambaye ni mama yangu pia.
14 Nisalimieni Asunkrito, Flegoni, Herme Patroba, Herma na ndugu wote walio pamoja nao.
15 Nisalimieni Filologo na Yulia, Nerea na dada yake, na Olumpa, pamoja na watu wote wa Mungu walio pamoja nao.
16 Salimianeni ninyi kwa ninyi kwa ishara ya upendo. Salamu kwenu kutoka kwa makanisa yote ya Kristo.
17 Ndugu zangu, nawasihi muwafichue wote wanaosababisha mafarakano na kuwafanya watu wengine waanguke, kinyume cha mafundisho mliyofundishwa. Jiepusheni na watu hao,
Warumi 16 in Biblia Takatifu

Warumi 16:1-17 in Biblia ya Kiswahili

1 Namkabidhi kwenu Fibi dada yetu, ambaye ni mtumishi wa kanisa ambalo liko Kenkrea,
2 ili kwamba mnaweza kumpokea katika Bwana. Fanyeni hivi katika kicho cha thamani cha waumini, na msimame pamoja naye katika jambo lolote atakalokuwa na uhitaji nalo. Maana yeye mwenyewe amekuwa mhudumu wa wengi, na kwa ajili yangu mwenyewe.
3 Msalimu Priska na Akila, watenda kazi pamoja nami katika Kristo Yesu,
4 ambao kwa maisha yangu waliyahatarisha maisha yao wenyewe. Ninatoa shukrani kwao, na siyo tu mimi, bali pia kwa makanisa yote ya mataifa.
5 Lisalimie kanisa ambalo liko nyumbani kwao. Msalimie Epanieto mpendwa wangu, ambaye ni mzaliwa wa kwanza wa Kristo katika Asia.
6 Msalimie Mariamu ambaye ametenda kazi kwa bidii kwa ajili yenu.
7 Msalimie Androniko na Yunia, jamaa zangu, na wafungwa pamoja nami. Ni wa muhimu miongoni mwa mitume, ambao pia walitangulia kumjua Kristo kabla yangu.
8 Msalimie Ampliato, mpendwa wangu katika Bwana.
9 Msalimie Urbano, mtenda kazi pamoja nami katika Kristo, na Stakisi mpendwa wangu.
10 Msalimie Apele, mwenye kukubaliwa katika Kristo. Wasalimie wote ambao walio katika nyumba ya Aristobulo.
11 Nisalimie Herodioni, jamaa yangu. Nisalimie wote walio katika nyumba ya Narkiso, ambao wako katika Bwana.
12 Nisalimie Trifaina na Trifosa, wanaotenda kazi kwa bidii katika Bwana. msalimie Persisi mpendwa, ambaye ametenda kazi zaidi kwa Bwana,
13 Nisalimie Rufo, aliyechaguliwa katika Bwana na mama yake na wangu.
14 Msalimie Asinkrito, Flegon, Herme, Patroba, Herma, na ndugu wote walio pamoja nao.
15 Nisalimie Filologo naYulia, Nerea na dada yake, na Olimpa, na waumini wote walio pamoja nao.
16 Nisalimie kila mmoja kwa busu takatifu. Makanisa yote katika Kristo yawasalimu.
17 Sasa nawasihi, ndugu, kutafakari juu ya hao ambao wanasababisha mgawanyiko na vipingamizi. Wanakwenda kinyume na mafundisho ambayo mmekwisha kujifunza. Geukeni mtoke kwao.
Warumi 16 in Biblia ya Kiswahili