Text copied!
CopyCompare
Biblia ya Kiswahili - 1Wafalme - 1Wafalme 2

1Wafalme 2:7-14

Help us?
Click on verse(s) to share them!
7Hata hivyo, uonyeshe utu kwa wana wa Barizilai Mgileadi, na uwaache wawe miongoni mwa wale wanaokula mezani kwako, kwa kuwa walikuja kwangu wakati nilipomkimbia ndugu yangu Absalomu.
8Tazama, Shimei mwana wa Gera yuko pamoja na wewe, Wabenjamini wa Bahurimu, walionilaani kwa laana ya fujo siku niliyoenda kwa Mahanaimu. Shimei alishuka kuja kuniona pale Yorodani, na nikamwapia kwa BWANA, nikisema, 'Sitawaua kwa upanga,'
9Kwa hiyo sasa usimwache aiepuke adhabu. Wewe ni mwenye hekima, na utajua jinsi itakavyokupasa kumtendea. Utakileta hicho kichwa chenye mvi chini kaburini.”
10Ndipo Daudi alipolala na mababu zake na alizikwa kwenye mji wa Daudi.
11Siku ambazo Daudi alitwala Israeli zilikuwani miaka arobaini. Alikuwa ametawala kwa miaka saba kule Hebroni na kwa miaka thelethini na tatu kule Yerusalemu.
12Kisha Sulemani akaketi kwenye kiti cha enzi cha baba yake Daudi, na utawala wake ulikuwa imara.
13Kisha Adoniya mwana wa Hagathi alikuja kwa Bathisheba mama wa Sulemani., Naye akamwuliza, “Je, unakuja kwa amani?” Naye akajiibu. “kwa amani.”
14Kisha akasema, “Nina jambo la kukuambia.” Naye akajibu, “Sema.”

Read 1Wafalme 21Wafalme 2
Compare 1Wafalme 2:7-141Wafalme 2:7-14