Text copied!
CopyCompare
Biblia ya Kiswahili - 1Wafalme - 1Wafalme 15

1Wafalme 15:21-29

Help us?
Click on verse(s) to share them!
21Ikawa Baasha aliposikia haya, akaacha kuijenga Rama akarudi Tirza.
22Kisha mfalme Asa akaitangazia Yuda yote. Hakuna aliyeachwa. Wakayabeba mawe na miti ya Rama ambayo Baasha alikuwa akijengea mji. Kisha mfalme Asa akavitumia hivyo vitu kuijenga Geba ya Benjamini na Mispa.
23Mambo mengine yanyohusu utawala wa Asa, uwezo wake wote, yote aliyofanya, na miji aliyoijenga, je, hayakuandikwa katika kitabu cha matukio ya wafalme wa Yuda? Lakini wakati wa uzee wake alipata ugonjwa wa miguu.
24Kisha Asa akalala na mababu zake na akazikwa pamoja nao katika mji wa Daudi baba yake. Yehoshafati mwanae akawa mfalme mahali pake.
25Nadabu mwana wa Yerobiamu alianza kutawala huko Israeli wakati wa mwaka wa pili wa Asa mfalme wa Yuda; Aliitawala Israeli kwa miaka miwili.
26Akafanya yaliyo maovu mbele y a macho ya BWANA naye akatembea katika njia ya baba yake, na katika dhambi yake, aliisababisha Israeli kufanya dhambi.
27Baasha mwana wa Ahiya, wa familia ya Isakari, akafanya hila dhidi ya Nadabu; Baasha akamwua huko Gibethoni, ambao ulikuwa mji wa Wafilisti, kwa kuwa Nadabu na Israeli walikuwa wakiuhusuru Gibethoni.
28Katika mwaka wa tatu wa Asa mfalme wa Yuda, Baasha alimwua Nadabu naye akawa mfalme mahali pake.
29Mara tu baad ya kuwa mfalme, Baasha aliwaua watu wote wa familia ya Yeroboamu. Hakumwacha hata mmoja wa uzao wa Yeroboamu awe hai; Kwa njia hii akawa ameuharibu ukoo wote wa kifalme, kama vile BWANA alivyokuwa amesema kupitia mtumishi wake Ahiya Mshilo,

Read 1Wafalme 151Wafalme 15
Compare 1Wafalme 15:21-291Wafalme 15:21-29