Text copied!
CopyCompare
Biblia ya Kiswahili - Waamuzi - Waamuzi 5

Waamuzi 5:7-14

Help us?
Click on verse(s) to share them!
7Kulikuwa na mashujaa wachache huko Israeli, mpaka mimi, Debora, nilipochukua amri- mama alichukua amri katika Israeli!
8Walichagua miungu mpya, kulikuwa na vita katika malango ya jiji lakini bado hapakuwa na ngao au mikuki iliyoonekana kati ya watu elfu arobaini nchini Israeli.
9Moyo wangu unawaendea wakuu wa Israeli, pamoja na watu ambao walijitolea -tunambariki Bwana kwa ajili yao!
10Fikiria juu ya hili- ninyi ambao hupanda punda weupe mmeketi kwenye mazulia, nanyi mnaotembea njiani.
11Sikiliza sauti za wale wanaoimba kwenye maeneo ya kutekea maji. Huko wanasema tena juu ya matendo ya haki ya Bwana, na matendo ya haki ya wapiganaji wake katika Israeli. Ndipo watu wa Bwana wakashuka kwenye malango ya mji.
12Amka, amka, Debora! Amka, amka, imba wimbo! Simama, Baraka, na uwakamate wafungwa wako, wewe mwana wa Abinoamu.
13Wale waliokoka wakaja chini kwa watu wenye nguvu; watu wa Bwana walikuja kwangu pamoja na mashujaa.
14Walikuja kutoka Efraimu, ambao mizizi yao iko katika Amaleki; watu wa Benyamini walikufuata. Wakuu wa Makiri walitoka, na kutoka Zebuloni wale wanaobeba fimbo ya afisa.

Read Waamuzi 5Waamuzi 5
Compare Waamuzi 5:7-14Waamuzi 5:7-14