Text copied!
CopyCompare
Biblia ya Kiswahili - Waamuzi - Waamuzi 5

Waamuzi 5:10-29

Help us?
Click on verse(s) to share them!
10Fikiria juu ya hili- ninyi ambao hupanda punda weupe mmeketi kwenye mazulia, nanyi mnaotembea njiani.
11Sikiliza sauti za wale wanaoimba kwenye maeneo ya kutekea maji. Huko wanasema tena juu ya matendo ya haki ya Bwana, na matendo ya haki ya wapiganaji wake katika Israeli. Ndipo watu wa Bwana wakashuka kwenye malango ya mji.
12Amka, amka, Debora! Amka, amka, imba wimbo! Simama, Baraka, na uwakamate wafungwa wako, wewe mwana wa Abinoamu.
13Wale waliokoka wakaja chini kwa watu wenye nguvu; watu wa Bwana walikuja kwangu pamoja na mashujaa.
14Walikuja kutoka Efraimu, ambao mizizi yao iko katika Amaleki; watu wa Benyamini walikufuata. Wakuu wa Makiri walitoka, na kutoka Zebuloni wale wanaobeba fimbo ya afisa.
15Na wakuu wangu katika Isakari walikuwa pamoja na Debora; na Isakari alikuwa na Baraka waliingia bobdeni kwa kasi chini ya amri yake. Miongoni mwa jamaa za Reubeni kulikuwa na utafutaji mkubwa wa moyo.
16Kwa nini uliketi katikati ya moto, ukisikiliza wachungaji wakipiga filimbi yao kwa makundi yao? Na kwa jamaa za Reubeni kulikuwa na utafutaji mkubwa wa moyo.
17Gileadi alikaa upande wa pili wa Yordani; na Dani, kwa nini alizunguka juu ya meli? Asheri alibakia pwani na akaishi karibu na bandari zake.
18Zabuloni lilikuwa kabila ambayo lingeweza kuhatarisha maisha yao mpaka kufikia kifo, Nafthali, pia, katika uwanja wa vita.
19Wafalme walikuja, wakapigana; wafalme wa Kanaani wakapigana huko Taanaki karibu na maji ya Megido. Lakini hawakuondoa fedha kama nyara.
20Nyota zilipigana kutoka mbinguni, kutoka katika njia zao za mbinguni zilipigana na Sisera
21Mto Kishoni uliwaondoa, mto ule wa kale, Mto Kishoni. Endelea mbele nafsi yangu, jipe nguvu!
22Kisha sauti za hofu za farasi-kupiga mbio, kupigana kwa watu wake wenye nguvu.
23'Ilaani Meroz!' asema malaika wa Bwana. 'Hakika walaani wenyeji wake!' Kwa sababu hawakuja kumsaidia Bwana, kumsaidia Bwana katika vita dhidi ya mashujaa wenye nguvu.
24Yaeli amebarikiawa zaidi kuliko wanawake wengine wote, Yaeli (mke wa Heberi Mkeni), amebarikiwa zaidi kuliko wanawake wote wanaoishi katika hema.
25Mtu yule aliomba maji, naye akampa maziwa; akamletea siagi katika sahani inayofaa kwa wakuu.
26Aliweka mkono wake kwenye kigingi cha hema, na mkono wake wa kuia katika nyundo ya mfanyakazi; kwa nyundo akampiga Sisera, alimpiga kichwani kwake. Aliligawanya fuvu lake vipande vipande wakati alipompiga pembeni ya kichwa chake.
27Akaanguka katikati ya miguu yake, akaanguka akalala pale. Kati ya miguu yake akaanguka. Mahali alipoanguka ni pale ambapo aliuawa kwa ukatili.
28Aliangalia dirishani - mama yake Sisera aliangalia kupitia kamba na akasema kwa huzuni, 'Kwa nini gari lakelimechelewa kuja? Kwa nini viboko vya farasi vinavyovuta magari yake vimechelewa?'
29Wafalme wake wenye hekima walijibu, na yeye mwenyewe akajibu jibu lile

Read Waamuzi 5Waamuzi 5
Compare Waamuzi 5:10-29Waamuzi 5:10-29