Text copied!
CopyCompare
Biblia ya Kiswahili - Mambo ya Walawi - Mambo ya Walawi 15

Mambo ya Walawi 15:27-33

Help us?
Click on verse(s) to share them!
27Na yeyote anayegusa kitu kati ya vitu hivyo atakuwa najisi; lazima yeye afue nguo zake na aoge mwenyewe kwenye maji, na atakuwa amenajisika mpaka jioni.
28Lakini kama mwanamke ametakasika katika kutokwa na damu, ndipo atahesabu kwaajili yake siku saba, baada ya hizo atakuwa safi.
29Katika siku ya nane atachukua kwake njiwa wawili au kinda wawili wa njiwa na atawaleta kwa kuhani pakuingilia hema ya mkutano.
30Huyo kuhani atatoa ndege mmoja kama sadaka ya dhambi na mwingine kama sadaka ya kuteketezwa, na atafanya upatanisho kwaajili ya huyo mbele ya Yahwe kwaajili unajisi wa mwanamke atokwaye damu.
31Hivi ndivyo lazima uwatenge watu wa Israeli katika unajisi wao, hivyo hawatakufa tokana na unajisi wao, kwa kuchafua hema langu, ambapo naishi kati yao.
32Huu ndio utaratibu kwa kila ambaye anakisonono, kwaajili kila mwanaume ambaye shahawa yake inatoka na inamfanya kuwa najisi,
33kwaajili ya mwanamke ambaye yuko katika kipindi cha hedhi, kwaajili ya yeyote aliye na kisonono, awe mwanaume au mwanamke, na kwaajili ya yeyote anayelala na mwanamke najisi.

Read Mambo ya Walawi 15Mambo ya Walawi 15
Compare Mambo ya Walawi 15:27-33Mambo ya Walawi 15:27-33