Text copied!
CopyCompare
Biblia ya Kiswahili - Luka - Luka 22

Luka 22:43-49

Help us?
Click on verse(s) to share them!
43Kisha malaika kutoka mbinguni akamtokea, akamtia nguvu.
44Akiwa katika kuugua, akaomba kwa dhati zaidi, na jasho lake likawa kama matone makubwa ya damu yakidondoka chini.
45Wakati alipoamka kutoka katika maombi yake, alikuja kwa wanafunzi, na akawakuta wamelala kwa sababu ya huzuni yao,
46na akawauliza, “Kwanini mnalala? Amkeni muombe, kwamba msiingie majaribuni.”
47Wakati alipokuwa bado akiongea, tazama, kundi kubwa la watu likatokea, na Yuda, mmoja wa mitume kumi na wawili akiwaongoza. Akaja karibu na Yesu ili ambusu,
48lakini Yesu akamwambia, “Yuda, je unamsaliti Mwana wa Adamu kwa busu?”
49Wakati wale waliokuwa karibu na Yesu walipoona hayo yanayotokea, wakasema, “Bwana, je tuwapige kwa upanga?”

Read Luka 22Luka 22
Compare Luka 22:43-49Luka 22:43-49