Text copied!
CopyCompare
Biblia ya Kiswahili - Luka - Luka 11

Luka 11:6-17

Help us?
Click on verse(s) to share them!
6Kwa sababu rafiki yangu amenijia sasa hivi kutoka safarini, nami sina cha kumuandalia.'
7Na yule aliyeko ndani akamjibu, usinitaabishe, Mlango umekwisha kufungwa, na watoto wangu, pamoja nami tumekwisha kulala kitandani. Siwezi kuamka na kukupa wewe mikate.
8Nawaambia, japo kuwa haamki na kukupatia mikate kama rafiki yake, kwa sababu ya kuendelea kumgongea bila aibu, ataamka na kukupatia vipande vingi vya mikate kulingana na mahitaji yako.
9Nami pia nawaambieni, Ombeni, nanyi mtapewa; tafuteni, nanyi mtapata, pigeni hodi nanyi mtafunguliwa.
10Kwa kuwa kila mtu aombaye atapokea, na kila mtu atafutaye atapata, na kila mtu apigaye hodi, mlango utafunguliwa kwake.
11Ni baba yupi miongoni mwenu, mwanaye akimuomba samaki atampa nyoka badala yake.?
12Au akimuomba yai atampa nge badala yake?.
13Kwa hiyo, ikiwa ninyi mlio waovu mnajuwa kuwapa watoto wenu zawadi nzuri, je si zaidi sana Baba yenu wa mbinguni kwamba atawapa Roho Mtakatifu hao wamuombao?”
14Baadaye, Yesu akawa anakemea pepo, na mtu mwenye pepo alikuwa bubu. Ikawa pepo lilipomtoka, mtu huyo aliweza kuongea. Umati wakastaajabu sana.
15Lakii watu wengine wakasema, huyu anaondo mapepo kwa Beelzebul, mkuu wa mapepo
16Wengine walimjaribu na kumtaka awaonyeshe ishara kutoka mbinguni.
17Lakini Yesu aliyatambua mawazo yao na kuwaambia, “Kila ufalme utakaogawanyika itakuwa ukiwa, na nyumba iliyo gawanyika itaanguka.

Read Luka 11Luka 11
Compare Luka 11:6-17Luka 11:6-17