Text copied!
CopyCompare
Biblia ya Kiswahili - 1Wafalme - 1Wafalme 16

1Wafalme 16:3-29

Help us?
Click on verse(s) to share them!
3Tazama, Nitamfagia kabisa Baasha na familia yake na nitaifanya familia yako kama familia ya Yeroboamu mwana wa Nebati.
4Mbwa watamla yeyote ambaye anatoka kwa Baasha wanaofia mjini, na ndege wa angani watamla yeyote anayaefia shambani.”
5Lakini kwa mambo mengine yanayohusiana na Baasha, aliyofanya, na uwezo wake, je, hayakuandikwa katika kitabu cha matukio ya wafalme wa Israeli?
6Baasha akalala na mababu zake na akazikwa Tirza, na Ela mwanae akawa mfalme mahali pake.
7Kwa kupitia nabii Yehu mwana wa Hanani neno la BWANA likaja kinyume na Baasha na familia yake, wote kwa sababu ya maovu yote aliyofanya machoni pa BWANA, akamghadhabisha kwa kazi ya mikono yake, kama familia ya Yeroboamu, na kwa sababu alikuwa ameiua familia yote ya Yeroboamu.
8Katika mwaka wa kumi na sita wa Asa mfalme wa Yuda, Ela mwana wa Baasha akaanza kutawala juu ya Israeli kule Tirza; akatawala kwa miaka miwili.
9Mtumishi wake Zimri, mkuu wa nusu ya magari yake akatengeneza hila dhidi yake. Wakati huo Ela alikuwa Tirza, akinywa na kulewa kwenye nyumba ya Arza, ambaye alikuwa mkuu wa watumishi wa nyumbani huko Tirza.
10Zimri akaiingia ndani, akamshambulia na kumwua, katika mwaka wa ishirini na saba wa Asa mfalme wa Yuda, naye akawa mfalme mahali pake.
11Zimri alipoaanza kutawala, mara tu baada ya kukaa kwenye kiti cha enzi, akawaua wanafamilia wote wa Baasha. Hakumwacha mtoto hata mmoja wa kiume, hakuna hata wa ndugu yake wala wa rafiki zake.
12Kwa hiyo Zimri aliingamiza familia yote ya Baasha, kama alivyokuwa ameambiwa kwa neno la BWANA, ambalo lilinenwa kinyume na Baasha na nabii Yehu,
13kwa dhambi zote za Baasha na za Ela mwanae ambazo walizifanya, ambazo kwazo waliisababisha Israeli kufanya dhambi, kiasi c ha kumghadhabisha BWANA, Mungu wa Israeli, kuzikasilikia sanamu zao.
14Kwa mambo mengine yanayohusiana na Ela, yote ambayo alifanya, je hayajaandikwa kwenye kitabu cha matukio ya wafalme wa Israeli?
15Katika mwaka wa ishirini na saba wa Asa mfalme wa Yuda, Zimri alitawala kwa siku saba tu kule Tirza. Jeshi likafanya kambi kule Gibethoni, ambao ni mji wa Wafilisti.
16Lile jeshi lililokuwa limeweka kambi kule lilisikika lilksema, “Zimri amepanga njama na amemwua mfalme.” Kwa hiyo siku hiyo hapo kambini, Israeli yote ikamtangaza Omri, mkuu wa jeshi, kuwa mfalme wa Israeli.
17Omri akapanda kutoka Gibethoni na Israeli yote pamoja naye, nao wakauhusuru Tirza.
18Kwa hiyoZimri alipoona kuwa mji umetekwa, akaingia kwenye ngome na akaivamia ikulu ya mfalme na kulichoma moto jengo lote pamoja na yeye; kwa hiyo akafa kwa moto.
19Hii ilikuwa ni kwa sababu ya dhambi alizofanya kwa kufanya maovu mbele ya macho ya BWANA, kwa kutembea katika njia ya Yeroboamu na katika dhambi ambazo alifanya, kiasi cha kuifanya Israeli wafanye dhambi.
20Pia kwa mambo mengiine yanayomhusu Zimri, na fitina yake aliyofanya, je, hayakuandikwa kwenye kitabu cha matukio ya wafalme wa Israeli?
21Sasa watu wa Israeli walikuwa wamegawanyika katika makundi mawili. Nusu ya watu walimfuata Tibni mwana wa Ginathi, wakamfanya kuwa mfalme, na Nusu walimfufata Omri.
22Lakini watu waliomfuata Omri walikuwa na nguvu kuliko wale waliomfuata Tibni mwana wa Ginathi. Kwa hiyo Tibni akafa, na Omri akawa mfalme.
23Omri alianza kutawala juu ya Israeli katika mwaka wa thelathini na moja wa Asa mfalme wa Yuda, naye akatawala miaka kumi na miwili. Alitawala akiwa Tirza kwa miaka sita.
24Akakinunua kilima cha Samaria kutoka kwa Shemeri kwa kilo 68 za fedha. Akajenga mji juu ya mlima na ule mji akauita Samaria, kwa sababu ya jina la Shemeri, mmiliki wa awali wa kile kilima.
25Omri akafanya maovu mbele ya BWANA na akafanya yaliyo maovu zaidi kuliko wale waliokuwa kabla yake.
26Kwa kuwa alitembea katika njia zote za Yeroboamu mwana wa Nebati na katika dhambi zake ambazo kwa hizo aliwaongoza Waisraeli kufanya dhambi, ili kumkasirisha BWANA, Mungu wa Israeli, ili kuwa na hasira juu ya sanamu zao za ubatili.
27Kwa mambo mengine yanayomhusu Omri ambayo alfanya, na nguvu zake alizoonyesha, je, hayakuandikwa katika kitabu cha matukio ya wafalme wa Israeli?
28Kwa hiyo Omri akalala na mababu zake na akazikwa Samaria na Ahabu mwanae akawa mfalme mahali pake.
29Katika mwaka wa thelathiini na nane wa Asa mfalme wa Yuda, Ahabu mwana wa Omri akaanza kutawala juu ya Israeli. Ahabu mwana wa Omri akatawala Israeli kule Samaria kwa miaka ishirini na mbili.

Read 1Wafalme 161Wafalme 16
Compare 1Wafalme 16:3-291Wafalme 16:3-29