3Na nyuma ya pazia la pili kulikuwa na chumba kingine, paliitwa mahali patakatifu zaidi.
4Mlikuwemo madhabahu ya dhahabu kwa kuvukizia uvumba. Pia mlikuwemo sanduku la agano, ambalo lilikuwa limejengwa kwa dhahabu tupu. Ndani yake kulikuwa na bakuli la dhahabu lenye manna, fimbo ya Haruni iliyoota majani, na zile mbao za mawe za agano.
5Juu ya sanduku la agano maumbo ya maserafi wa utukufu wafunika mabawa yao mbele ya kiti cha upatanisho, ambacho kwa sasa hatuwezi kuelezea kwa kina.
6Baada ya vitu hivi kuwa vimekwisha andaliwa, Makuhani kawaida huingia chumba cha nje cha hema kutoa huduma zao.
7Lakini kuhani mkuu huingia kile chumba cha pili pekee mara moja kila mwaka, na pasipo kuacha kutoa dhabihu kwa ajili yake binafsi, na kwa dhambi za watu walizozitenda pasipo kukusudia.
8Roho Mtakatifu anashuhudia kwamba, njia ya mahali patakatifu zaidi bado haijafunuliwa kwa vile ile hema la kwanza bado linasimama.
9Hili ni kielelezo cha muda huu wa sasa. Vyote zawadi na dhabihu ambavyo vinatolewa sasa haviwezi kukamilisha dhamiri ya anayeabudu.
10Ni vyakula na vinywaji pekee vimeunganishwa katika namna ya taratibu za ibada ya kujiosha. Vyote hivi vilikuwa taratibu za kimwili vilivyokuwa vimeandaliwa hadi ije amri mpya itakayowekwa mahali pake.
11Kristo alikuja kama kuhani mkuu wa mambo mazuri ambayo yamekuja. kupitia ukuu na ukamilifu wa hema kuu ambayo haikufanywa na mikono ya watu, ambayo si wa ulimwengu huu ulioumbwa.
12Ilikuwa si kwa damu ya mbuzi na ndama, bali kwa damu yake mwenyewe kwamba Kristo aliingia mahali patakatifu zaidi mara moja kwa kila mmoja na kutuhakikishia ukombozi wetu wa milele.