1Ilikuwa hivi Melkizedeki, mfalme wa Salemu, Kuhani wa Mungu aliye juu, aliyekutana na Abrahamu akirudi kutoka kuwaua wafalme na akambariki.
2Abrahamu alimpa moja ya kumi ya kila kitu alichokuwa amekiteka. Jina lake “Melkizedeki “maana yake” mfalme wa haki” na pia “mflame wa Salemu” ambayo ni “mfalme wa amani.”
3Hana baba, hana mama, hana wazazi, hana mwanzo wa siku wala mwisho wa maisha yake. Badala yake, anabakia kuhani milele, kama mwana wa Mungu.
4Sasa fikiria jinsi huyu mtu alivyokuwa mkuu. Mzazi wetu Abrahamu alimpa moja ya kumi ya vitu vizuri alivyovichukua vitani.
5Na hakika, ukoo wa Walawi waliopokea ofisi za kikuhani walikuwa na amri kutoka kwenye sheria kukusanya moja ya kumi kutoka kwa watu, ambayo ni, kutoka kwa Wairaeli wenzao, pamoja na kwamba wao, pia, ni ukoo kutoka kwa Abrahamu.
6Lakini Melkizedeki, ambaye hakuwa wa ukoo kutoka kwa Walawi, alipokea moja ya kumi kutoka kwa Abrahamu, na akambariki, yeye aliyekuwa na ahadi.
7Hapo haikataliwi kwamba mtu mdogo hubarikiwa na mkubwa.
8Kwa jambo hili mtu apokeaye moja ya kumi atakufa siku moja, lakini kwa jambo jingine mmoja aliyepokea moja ya kumi kwa Abrahamu ikaelezwa kama anayeishi.
9Na kwa namna ya kuzungumza, Lawi aliyepokea moja ya kumi, pia alilipa moja ya kumi kwa Abrahamu,
10kwa sababu Lawi alikuwa katika viuno vya baba yake Abrahamu wakati Melkizedeki alipokutana na Abrahamu.
11Sasa kama ukamilifu uliwezekana kupitia ukuhani wa Lawi, (hivyo chini yake watu hupokea sheria), kulikuwa na hitaji gani zaidi kwa kuhani mwingine kuinuka baada ya mfumo wa Melkizedeki, na siyo kuitwa baada ya mpangilio wa Haruni?
12Kwa hiyo ukuhani ukibadilika, hapana budi sheria nayo kubadilika.
13Kwa mmoja ambaye mambo haya yalisemwa kuhusu kabila jingine, kutoka kwake hakuna aliyehudumu madhabahuni.
14Sasa ni wazi kwamba Bwana wetu alitoka katika Yuda, kabila ambalo Musa hakutaja kuhusu makuhani.
15Na haya tusemayo ni wazi hasa ikiwa kuhani mwingine atatokea kwa mfano wa Melkizedeki.
16Kuhani huyu mpya siyo mmoja ambaye amekuwa kuhani juu ya msingi wa sheria zinazohusiana na uzao wa mtu, lakini katika msingi wa nguvu ya maisha yasiyoweza kuharibika.
17Hivyo maandiko yanashuhudia kuhusu yeye: “Wewe ni kuhani milele baada ya mfumo wa Melkizedeki.”
18Kwa kuwa amri iliyotangulia iliwekwa pembeni kwa sababu ilikuwa dhaifu na haifai.
19Hivyo sheria haikufanya chochote kikamilifu. Isipokuwa, kulikuwa na ujasiri mzuri kwa hayo tunamsogelea Mungu.
20Na Ujasiri huu mzuri haukutokea pasipo kuzungumzia kiapo, kwa hili makuhani wengine hawakuchukua kiapo chochote.
21Lakini Mungu alichukua kiapo wakati aliposema kuhusu Yesu, “Bwana ameapa na hatabadilisha mawazo yake.' wewe ni kuhani milele.”
22Kwa hili Yesu pia amekuja kuwa dhamana ya agano bora.
23Kwa hakika, kifo huzuia makuhani kuhudumu milele. Hii ni kwa sababu walikuwapo makuhani wengi, mmoja baada ya mwingine.
24Lakini kwa sababu Yesu anaishi milele, ukuhani wake haubadiliki.
25Kwa hiyo yeye pia anaweza kwa ukamilifu kukamilisha kuwaokoa wanaomkaribia Mungu kupitia kwake, kwa kuwa yeye anaishi daima kwa kuomba kwa ajili yao.
26Kwa hiyo kuhani mkuu wa namna hii anastahili kwetu. Asiye na dhambi, hatia, msafi, aliyetengwa kutoka kwa wenye dhambi, na amekuwa juu kuliko mbingu.
27Yeye hakuwa na uhitaji, mfano wa makuhani wakuu, kutoa dhabihu kila siku, kwanza kwa dhambi yake mwenyewe, na baadaye kwa dhambi za watu. Alifanya hivi mara moja kwa wote, alipojitoa yeye mwenyewe.
28Kwa sheria huwateua watu dhaifu kuwa makuhani wakuu, lakini neno la kiapo, lililokuja baada ya sheria, alimteua Mwana, aliyefanywa kuwa mkamilifu milele.