Text copied!
CopyCompare
Biblia ya Kiswahili - Wahebrania

Wahebrania 4

Help us?
Click on verse(s) to share them!
1Kwa hiyo, tunapaswa kuwa makini ili kwamba kati yenu asiwepo hata mmoja atakayeonekana kushindwa kufikia ahadi endelevu ya kuingia katika pumzika la Mungu.
2Kwani tumekuwa na habari njema kuhusu pumziko la Mungu lililotangazwa kwetu kama Waisrael walivyokuwa nayo, lakini ujumbe huo haukuwasaidia wale ambao waliusikia bila kuunganisha imani kwa hilo.
3Kwa sisi, ambao tumekwisha amini-sisi ndio miongoni tutakaoingia katika lile pumuziko, Kama inavyosema, “Kama nilivyoapa kwa hasira yangu, Hawataingia katika pumziko mwangu.” Alisema hili, ingawa kazi zote alizotengeneza zilikuwa zimekamilika tangu mwanzo wa ulimwengu.
4Kwani ameshasema sehemu fulani kuhusu siku ya saba, “Mungu alipumzika siku ya saba katika yote aliyoyafanya.”
5Tena ameshasema, “Hawataingia kwenye pumziko langu.”
6Kwa sababu hiyo, tangu pumziko la Mungu bado ni akiba kwa ajili ya baadhi kuingia, na tangu Waisraeli wengi ambao walisikia habari njema kuhusu pumziko lake hawakuingia kwa sababu ya kutotii,
7Mungu aliweka tena siku fulani, iitwayo “Leo.” Yeye aliiongeza siku hii alipozungumza kupitia Daudi, ambaye alisema kwa muda mrefu baada ya yaliyosemwa kwanza, “Leo kama mtasikia sauti yake, msifanye mioyo yenu kuwa migumu.”
8Kwani kama Yoshua aliwapatia pumziko, Mungu asingelisema juu ya siku nyingine.
9Kwa hiyo bado kuna Sabato ya pumziko iliyotunzwa kwa ajili ya watu wa Mungu.
10Kwani anayeingia katika pumziko la Mungu yeye mwenyewe pia amepumzika kutokana na matendo yake, kama Mungu alivyofanya katika yeye.
11Kwa hiyo tuweni na shauku ya kuingia katika lile pumziko, ili kwamba asiwepo atakayeanguka katika aina ya uasi waliofanya.
12Kwa maana neno la Mungu li hai na lina nguvu na linaukali kuliko upanga wowote wenye makali kuwili. Na huchoma hata kufikia kugawanya nafsi na roho, na viungo kutika uboho. Na lenye kuweza kufahamu fikira za moyo nia yake.
13Hakuna kilichoumbwa kilichojificha katika uso wa Mungu. Badala yake, kila kitu ni dhahiri na wazi kwa macho ya mmoja ambaye ni lazima tutoe hesabu.
14Baadaye kuwa na kuhani mkuu aliyeingia katika mbingu, Yesu Mwana wa Mungu, kwa uimara tushikilie imani zetu.
15Kwa kuwa hatuna kuhani mkuu ambaye hawezi kuhisi huruma kwa ajili udhaifu wetu, lakini yeye ambaye kwa njia zote amekuwa akijaribiwa kama sisi, isipokuwa yeye ambaye hana dhambi.
16Na tuje kwa ujasiri katika kiti cha enzi cha neema, ili kwamba tupokee rehema na kupata neema ya kutusaidia wakati wa hitaji.