1Kwa hiyo, ndugu watakatifu, washiriki wa wito wa mbinguni, mumfikiri Yesu, Mtume na Kuhani Mkuu wa ukiri wetu.
2Alikuwa mwaminifu kwa Mungu aliyemteua, kama Musa alivyokuwa mwaminifu pia katika nyumba yote ya Mungu.
3Kwa kuwa Yesu amehesabiwa kuwa na heshima kubwa kuliko aliyokuwa nayo Musa, kwa sababu yule anayejenga nyumba anahesabiwa kuwa na heshima kubwa kuliko nyumba yenyewe.
4Kwa kuwa kila nyumba hujengwa na mtu fulani, lakini yule anayejenga kila kitu ni Mungu.
5Hakika Musa alikuwa mwaminifu kama mtumishi katika nyumba yote ya Mungu, akitoa ushuhuda kuhusu mambo yatakayosemwa wakati ujao.
6Lakini Kristo ni Mwana katika usimamizi wa nyumba ya Mungu. Sisi ni nyumba yake kama tutashikilia haraka katika kujiamini na fahari ya kujiamini.
7Kwa hiyo, ni kama Roho Mtakatifu asemavyo, “Leo, kama utasikia sauti yake,
8Usiufanye moyo wako kuwa mgumu kama Waisraeli walivyofanya katika uasi, katika wakati wa kujaribiwa nyikani.
9Huu ulikuwa wakati ambao baba zenu waliniasi kwa kunijaribu, na wakati, kwa miaka arobaini, waliona matendo yangu.
10Kwa hiyo sikufurahishwa na kizazi hicho. Nilisema, 'Wanapotea kila mara katika mioyo yao, na hawajui njia zangu.
11Ni kama vile nilivyoapa katika hasira yangu: hawataiingia raha yangu.”
12Muwe waangalifu, ndugu, ili kwamba usije ukawepo moyo mwovu wa kutokuamini kwa mmoja wenu, moyo ambao utakwenda mbali na Mungu aliye hai.
13Badala yake, mhamasishane kila siku kila mmoja na mwenzie, ili kila iitwapo leo mtamani, ili kwamba mmoja kati yenu asifanywe kuwa mgumu kwa udanganyifu wa dhambi.
14Kwa maana tumekuwa washiriki wa Kristo ikiwa tutashikamana na uthabiti wetu kwa nguvu katika yeye kutoka mwanzo hadi mwisho.
15Kuhusu hili imekwisha kusemwa, “Leo kama mtaisikiliza sauti yake, msiifanye mioyo yenu kuwa migumu, kama Waisraeli walivyofanya wakati wa uasi.”
16Ni akina nani hao waliomsikia Mungu na kuasi? Hawakuwa wale wote ambao Musa alikuwa amewaongoza kutoka Misri?
17Na kina nani ambao Mungu aliwakasirikia kwa miaka arobaini? Siyo pamoja na wale waliotenda dhambi, ambao miili yao iliyokufa ililala jangwani?
18Ni akina nani aliowaapia Mungu kwamba hawataingia katika raha yake, kama siyo wale ambao hawakumtii yeye?
19Tunaona kwamba hawakuweza kuingia katika raha yake kwa sababu ya kutokuamini.