Text copied!
CopyCompare
Biblia ya Kiswahili - 1Wafalme - 1Wafalme 2

1Wafalme 2:12-21

Help us?
Click on verse(s) to share them!
12Kisha Sulemani akaketi kwenye kiti cha enzi cha baba yake Daudi, na utawala wake ulikuwa imara.
13Kisha Adoniya mwana wa Hagathi alikuja kwa Bathisheba mama wa Sulemani., Naye akamwuliza, “Je, unakuja kwa amani?” Naye akajiibu. “kwa amani.”
14Kisha akasema, “Nina jambo la kukuambia.” Naye akajibu, “Sema.”
15Adoniya amesema, “Unajua kuwa ufalme ulikuwa wangu, na kwamba Israeli yote ilikuwa inanitegemea mimi kuwa mfalme. Hata hivyo, ufalme umegeuzwa na umekuwa wa ndugu yangu, kwani ulikuwa wake toka kwa BWANA.
16Sasa nina ombi moja kwako. Usinikatalie.” Bathisheba akamwambia, “Sema.”
17Naye akamwambia, “Tafadhali mwambie mfalme Sulemani, kwa kuwa hatakukatalia, ili kwamba anipatie Abishagi Mshunami awe mke wangu.”
18Bathisheba akamwambia, “Vyema sana, nitamwambia mfalme”
19Kwa hiyo Bathisheba akaenda kumwambia, mfalme Sulemani kwa niaba ya Adoniya. Mfalme akainuka kumlaki na akapiga magoti mbele yake. Kisha akaa kwenye kiti chake cha enzi na kulikuwa na kiti kingine cha enzi kilicholetwa kwa ajili ya mama wa mfalme. Naye akaa mkono wa kuume wa mfalme.
20Ndipo alipomwambia, “Napenda kukuomba ombi moja dogo. Usinikalie.” Mfalme, akamjibu, “Mama omba kwa kuwa sitakukatalia.”
21Naya akamwambia, “Naomba Abishagi Mshunami apewe Adoniya ndugu yako awe mke wake.”

Read 1Wafalme 21Wafalme 2
Compare 1Wafalme 2:12-211Wafalme 2:12-21