Text copied!
CopyCompare
Biblia Takatifu - Yohana - Yohana 3

Yohana 3:31-35

Help us?
Click on verse(s) to share them!
31“Anayekuja kutoka juu ni mkuu kuliko wote; atokaye duniani ni wa dunia, na huongea mambo ya kidunia. Lakini anayekuja kutoka mbinguni ni mkuu kuliko wote.
32Yeye husema yale aliyoyaona na kuyasikia, lakini hakuna mtu anayekubali ujumbe wake.
33Lakini mtu yeyote anayekubali ujumbe wake anathibitisha kwamba Mungu ni kweli.
34Yule aliyetumwa na Mungu husema maneno ya Mungu, maana Mungu humjalia mtu huyo Roho wake bila kipimo.
35Baba anampenda Mwana na amemkabidhi vitu vyote.

Read Yohana 3Yohana 3
Compare Yohana 3:31-35Yohana 3:31-35